Rais Samia katika mapinduzi kidijitali na diplomasia ya uchumi

Rais Samia katika mapinduzi kidijitali na diplomasia ya uchumi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Baada ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaleta nchini Tanzania wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka katika nchi 27 (Mwezi August 2022) wanaojishughulisha na mambo ya TEHAMA na kufungua fursa za uwekezaji katika mawanda ya kidijiti.

Mwishoni mwa Mwezi ujao (OKTOBA) wafanyabiashara na wadau wa TEHAMA wa Tanzania wanakwenda nchini Congo DRC, kwaajili ya mkutano wa kibiashara unaolenga kufungua fursa lukuki .

Kwa Kumbukumbu, DRC ni soko lenye ukubwa wa zaidi ya watu Milioni 95. Mwenye macho haambiwi tazama.
Fursa za uwekezaji, fursa za soko kubwa, milango ya biashara na uwekezaji inazidi kufunguliwa kila uchao.
Ni jukumu lako sasa kuzitumia ili kutengeneza ajira, kulipa kodi ya kujenga nchi yako na kustawisha maisha yako binafsi.

Muda ni sasa! Utekelezaji wa sera ya mambo ya nje inayochagiza Diplomasia ya uchumi sanjari na kutumia fursa za mageuzi ya kidijitali inakwenda kumnufaisha kila mtanzania aliyejipanga tayari kutumia fursa. Hongera Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri iliyotukuka.
 
Back
Top Bottom