Wadau, niko Tanga mjini hapa na katika pitapita zangu nimekutana na vijana wakizungumza kwa furaha kwamba kesho hakuna shule ni mapumziko. Nikafikiri nimepitwa na nyakati kuna holiday halafu sijui, nikamuuliza kijana mmoja kwa nini hakuna shule akanijibu mwalimu mkuu kawatangazia kuwa rais Samia anahutubia kwa hiyo wasiende shule.
Nina ndugu yangu mwalimu tena mwalimu mkuu wa shule moja ya msingi hapa mjini nikamuuliza kulikoni, akanijibu afisa elimu kawaambia kesho hakuna kwenda kufundisha walimu wote wa manispaa ya Tanga mjini wanatakiwa kuwa uwanjani Mkwakwani bila kukosa sababu mheshimiwa Rais atakuwa anahutubia.
Inawezekana mimi sina akili nawaza rais kuhutubia wanafunzi wasifundishwe? Na walimu wasiende kazini waende wakajaze uwanja kwa mama anayeupiga mwingi?
Serikali ya CCM yenye rais anayeupiga mwingi, anayependwa sana inalazimisha walimu wakajae uwanjani badala ya kwenda kazini kuwafundisha watoto?
Naomba kusahihishwa hii ni sawa au mimi ndio nimechanganyikiwa?