Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Mh Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa amenukuliwa vibaya kwani rufaa ni utaratibu wa kisheria. Na baada ya maamuzi ya Mh Rais kama mhusika hajarizika sheria inamruhusu kwenda Mahakani.
Sheria gani inayomruhusu kwenda mahakamani baada ya uamuzi wa Rais?
 
Amekataa rufaa wapi? Kwa maneno gani?

Nimeomba maneno halisi aliyoyatoa rais hapa, mpaka sasa sijayaona.

Naona tafsiri za watu za maneno ambayo kasema rais.

That is hearsay.Hata mahakamani sehemu nyingi hawaruhusu hearsay.

Maneno halisi aliyosema rais ni yapi?
Mliotaka video, hiyo hapo. Anzia Dakika ya 20:45 na/ au dakika ya 21:20, Rufaa za kipumbavu pumbavu

Kwani sheria inasemaje?

Kisheria watu wanaruhusiwa kukata rufaa kwa rais?
Kisheria, rufaa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma inapelekwa kwa Mhe. Rais. Kwa kuwa watumishi wataendelea kufuata sheria, rufaa zitaendelea kupelekwa kwa Mhe. Rais. Labda kama rufaa husika 'hazitafika' au kufanikiwa ziendako.
 
Rais kasema anakataa rufaa za kipumbavupumbavu.

Wewe unazikubali?
 
Rais kasema anakataa rufaa za kipumbavupumbavu.

Wewe unazikubali?
Mkuu, Rufaa ni Rufaa, ikiwa haina makosa katika uandishi wake, inapaswa kupokelewa na kusikilizwa. Umaana au upumbavu wa rufaa utagundulika baada ya kuipitia/kusikiliza rufaa husika. Ukikataa kuzipokea kwa sababu kwa utashi wako umeziona ni za 'kipumbavu pumbavu' hapo unakuwa umekiuka Sheria. Pokea, Sikiliza halafu toa maamuzi kuwa hii Rufaa ni ya Kipumbavu pumbavu.
 
Fuatilia wapo watu wameshinda rufaa zao tume na kurejeshwa kazini na kulipwa stahiki zao zote, ukiona hilo halijafanyika ujue huyo mtu hakustahili. Mambo yote yanafanyika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Watu kushinda Rufaa na kurejeshwa kazini au kulipwa stahiki zao haimaanishi kuwa mambo yamefanyika kwa mujibu wa STK kama ulivyosema. Sheria na kanuni zinasema TUME wanatakiwa kusikiliza na kutoa uamuzi wa Rufaa ndani ya siku 90 toka kuwasilishwa kwake, je umeona suala hilo likitekelezwa? Je, si kweli kuwa Rufaa zinakaa huko tume mpaka miaka miwili au mitatu ndio zinatolewa uamuzi?
 
Mkuu, Rufaa ni Rufaa, ikiwa haina makosa katika uandishi wake, inapaswa kupokelewa na kusikilizwa. Umaana au upumbavu wa rufaa utagundulika baada ya kuipitia/kusikiliza rufaa husika. Ukikataa kuzipokea kwa sababu kwa utashi wako umeziona ni za 'kipumbavu pumbavu' hapo unakuwa umekiuka Sheria. Pokea, Sikiliza halafu toa maamuzi kuwa hii Rufaa ni ya Kipumbavu pumbavu.
Rais ana haki ya kukataa rufaa za kipumbavu.

Alichokosea ni kutotumia mikono ya taasisi ya urais kufanya hilo.

Kama vile kila rufaa inabidi aipitie yeye.

Wakati angeweza kuweka mfumo wa kuchuja rufaa ili yeye zimfikie zenye umuhimu tu.

Labda kashafundishwa na mwendazake kwamba ukiwa rais, washauri wako hawajui kitu.
 
Labda ungeeleza maana ya kukataa.
Ikiwa maana ya neno kukataa unaichukulia as in , 'Rufaa ya mtumishi ... imekataliwa (dismissed) kwa kukosa sababu za kuridhisha' hapo uko sahihi, ILA kama kukataa unamaanisha kuwa,
Rais: Hiyo rufaa inahusu nini?
KMK: Utoro kazini
Rais;Tupa kule, sitaki Rufaa za kipumbavupumbavu mimi, Hapo basi unakuwa haupo sahihi.

Rais ana mamlaka ya kukataa Rufaa kisheria na atapaswa kutoa sababu za kisheria za kwa nini amekataa Rufaa hiyo na sio kwa maneno matupu tu. Mfano aliotoa kuwa mtu hayupo kazini wiki 2 bila Taarifa akifukuzwa kazi akate rufaa halafu ije kwake anaiita ya kipumbavupumbavu, vipi kama huyo mtu analalamika kuwa utaratibu wa kumfukuza kazi haukufuatwa? kwamba hakusikilizwa ili aeleze ni kwa nini hakutoa taarifa za kutokuwepo kwake? Au kwamba alitoa taarifa lakini ilipuuzwa, sasa analalamika kuwa alitoa taarifa na sio kama asemavyo mwajiri kuwa hakutoa taarifa, hizo unaitaje rufaa za kipumbavupumbavu?

Upumbavu wa Rufaa unapaswa kuonekana kwenye maamuzi ya rufaa na sio wakati wa uwasilishwaji wa Rufaa au vinginevyo.
 
Ana maanisha wanapaswa wafanye kazi zao kwa haki na utaratibu uliyopangwa...
 
Back
Top Bottom