Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Kisheria, rufaa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma inapelekwa kwa Mhe. Rais. Kwa kuwa watumishi wataendelea kufuata sheria, rufaa zitaendelea kupelekwa kwa Mhe. Rais. Labda kama rufaa husika 'hazitafika' au kufanikiwa ziendako.

Nadhani Tume haiko independent,Inaogopa Gharama kama Mtumishi Ana Haki...Yaani Kurejeshewa stahiki zake...
Wanaona hiyo hasara italipa Serikali,Na Serikali inawakilishwa na Tume!
 
Nadhani Tume haiko independent,Inaogopa Gharama kama Mtumishi Ana Haki...Yaani Kurejeshewa stahiki zake...
Wanaona hiyo hasara italipa Serikali,Na Serikali inawakilishwa na Tume!
Hapo ndo wanapoharibu kabisaaaa!!!

Kama Tume haitaki kutoa haki kisa wanaogopa gharama kwa Serikali pindi mtumishi anaposhinda kesi, this is totally wrong!!!

Kama ni hivyo basi hakuna haja na kuwa na ofisi ya Tume, ni bora ifisi ya Tume ifungwe maana inaonekana wanapata mshahara wa bure.

Basi kama ni hivyo uendelee kusimama uamuzi wa mwajiri if that's the case ili kuondoa duplication of efforts maana ofisi ya Tume haina maana tena, ni kama rubber stamp na kuliongezea Taifa gharama za bure kwa kuwalipa mshahara.
 
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
Kama hajaweka angalizo la kesi kukatiwa rufaa m ahakamani kama mtumishi hajaridhika na maamuzi ya tume, ni hatari. Mabalaza ya kazi na time ni wapokeaji wakubwa wa hongo toka kwa waajiri ili kukandamiza haki za watumishi.
 
Hapo ndo wanapoharibu kabisaaaa!!!

Kama Tume haitaki kutoa haki kisa wanaogopa gharama kwa Serikali pindi mtumishi anaposhinda kesi, this is totally wrong!!!

Kama ni hivyo basi hakuna haja na kuwa na ofisi ya Tume, ni bora ifisi ya Tume ifungwe maana inaonekana wanapata mshahara wa bure.

Basi kama ni hivyo uendelee kusimama uamuzi wa mwajiri if that's the case ili kuondoa duplication of efforts maana ofisi ya Tume haina maana tena, ni kama rubber stamp na kuliongezea Taifa gharama za bure kwa kuwalipa mshahara.
It is very unfair kwa Tume kukaa na rufaa ya Mtumishi say, mwaka au miaka halafu wanakuja na majibu ya hovyo and very discouraging kwa Mtumishi wakati rufaa yake ina merit kisa wanaogopa gharama, hii ni dhambi kubwa sana mbele ya mwenyezi Mungu kwa kupoka haki ya mtu.
 
magufuli tunakubaliana kuna mazuri amefanya ila tu mabaya ni mengi mno na mazito. elewa hilo kwanza.
Pili , hebu eleza mwisho wa kesi za utumishi katika mhusika kutafuta haki ni wapi? tuanzie hapo
Kesi za utumishi wa umma mwisho wake inapaswa kuwa mwajiri namba moja wa utumishi wa umma naye ni Rais. Ili kumrahisishia kazi yake kuna vyombo vinavyodadavua kesi hizo na kumpa Rais mapendekezo katika kufanya maamuzi yake. Sasa Rais Samia kasema yeye hatakwenda kinyume na mapendekezo (maamuzi) ya vyombo vyake. Kuna ubaya katika hilo?
 
Huyu mama akae akijua kwamba huu ni muhula wake wa kwanza na mwisho....haendi miaka 5 mingine...
 
Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
Kama ndivyo unavyodhani, anakwepaje jukumu la kikatiba la kuamua rufaa za watumishi kama anavyoelekezwa na katiba aliyoapa kuuiinda na kuifuata?
Asikwepe majukumu yake na kama aliona haliwezi Basi, ampeleke mswada bungeni wakirekebishe hicho kifungu na kukitoa kwenye mamlaka yake kiende kwa waziri wa kazi!
 
Magufuli alikuwa mchamungu feki, alikuwa kwenye msafara wake anaenda na kundi la waganga, wasukuma washamba sana nyinyi
Wewe bwege tu utaendelea kumuota Hayati Magufuli mpaka kifo chako kwa kuwa alikufanya mbaya sana na uuza madawa wako.
 
Wewe bwege tu utaendelea kumuota Hayati Magufuli mpaka kifo chako kwa kuwa alikufanya mbaya sana na uuza madawa wako.
yaani mimi nimuote dikteta,labda nimuote akiwa anateketea kwa moto ,
We unadhani kila mtu alikuwepo nchini wakati wa utawala dikteta fisadi
 
Wewe bwege tu utaendelea kumuota Hayati Magufuli mpaka kifo chako kwa kuwa alikufanya mbaya sana na uuza madawa wako.
Nyie misukule wake ndio mtapata tabu sana, sasaivi hakuna Tena buku Saba kenge nyinyi,,

Mama hataki wanafiki sasaivi
 
yaani mimi nimuote dikteta,labda nimuote akiwa anateketea kwa moto ,
We unadhani kila mtu alikuwepo nchini wakati wa utawala dikteta fisadi
Una nini wewe nyumbu? Michango yako tu humu JF inaonekana ulivyo utopolo pole sana!
 
Wewe bwege tu utaendelea kumuota Hayati Magufuli mpaka kifo chako kwa kuwa alikufanya mbaya sana na uuza madawa wako.
Magufuli ndiye aliyedababisha kesi nyingi za madai dhidi ya Serikali kwa kuwa alikuwa siyo mtu anayefuata taratibu katika kuwachisha watumishi kazi. Tanzania hatamsahau kwa UDIKTETA wake
 
Sheria inasema watumishibwana hakinyabkukata rufaa kwa rais.

Rais akikataa kusikikiza rufaa za watumishi, amewanyima haki.

Sasa ukisema "buruta mahakamani mpaka haki ipatikane" wakati mchakatobwa kupata haki unaruhusu rufaa kwa rais, unajichanganya.

Unanikumbusha msemo mmoja wa kabaila wa Marekani Henry Ford.

Henry Fird alikuwa na kiwanda cha magari Ford. Alitengeneza magari akauza kwa bei rahisi.

Tatizo lake magari yake yote meusi. Hayana rangi nyingine.

Watu wakawa wanamuuliza, tunaweza kupata magari ya rangi yoyote tunayotaka?

Akawajibu, mnaweza kupata rangi yoyote mnayotaka, ikiwa rangi mnayotaka ni nyeusi.

Sasa na wewe hapa umekuja na habari kama za Henry Ford.

Unataka watu wapate haki, ikiwa tu haki inataka mahakamani.

Kuna mchakato unaoruhusu rufaa kwa rais.
Rais yupi sasa Mkuu? Huyuhuyu aliyekataa hizo rufaa au mwingine? Lipo genge potoshaji "baadhi ya washauri" lina maslahi na hicho alichokikataa Mh. Rais hapo lazima kuidai haki kwa njia nyingine ili Rais atambue kuwa "...ala kumbe nilipotoshwa!" Ni ushauri wangu tu Mkuu kuchagua gari nyeusi ama kutochagua...
 
Amekataa rufaa wapi? Kwa maneno gani?

Nimeomba maneno halisi aliyoyatoa rais hapa, mpaka sasa sijayaona.

Naona tafsiri za watu za maneno ambayo kasema rais.

That is hearsay.Hata mahakamani sehemu nyingi hawaruhusu hearsay.

Maneno halisi aliyosema rais ni yapi?
 
Wewe mbwiga uraisi ni Taasisi, hujui usemalo. Lazima sheria na taratibu zichukue mkondo wake.
Kwani mahakama hazitoi haki? Au inakatazwa mtumishi kupeleka mashtaka kortini ili kudai haki yake iliyoporwa?
Ikiwa Rais atafanya kazi zote basi hatuna haja ya kuwa na mahakama wala idara zingine...
Hivi kwanini hatujui njia zenye afya kwa kudai haki zetu badala yake tunataka wanasiasa ndio watatue matatizo? Au ndivyo tulivyolelewa?
Haki haiombwi...
 
Back
Top Bottom