Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Kama seria unasema rufaa iende kwa rais , hakuna jinsi mama azipokee na azitolee maamuzi. There is no way mhe. Mama Rais wa JMT akwepe utekelezaji wa sheria iliyotungwa na bunge,itakuwa ni ukiukwaji wa katiba. Ninajiuliza kama marais walipoita wangesoma mahakama ikishahukumu mtu anyongwe , msilete faili mezani kwangu kusubiri msamaha wa rais,ni wananchi wengi wangeishanyongwa. Lakini sheria ilitungwa vile wakijua rais kama binadamu anaweza akamhurumia mkosaji. Lakini kubwa zaidi kesi ya mtumishi wa umma dhidi ya mwajiri ni ya watu wawili ambapo mwajiri ni mwenyenacho na mtumishi asiyekuwa nacho . Matokeo ni kuwa mtumishi ataminywa tu . Duniani anasadikiwa ni 3 asilimia ya binadamu hawawezi kula rushwa na kupindisha sheria majjaji wakiwemo. Rais asikwepe kupokea na kutoa misamaha akijridhisha mnyonge akionewa .Kwanza uongozi bora ni pale ubinadamu unapotumika kupendelea mnyonge kuliko uache sheia ichukue mkondo, mwanasiasa mahiri kama Samia asijinyime fursa ya kusomesha ubinadamu wake. Akikaa na na washauri wake abao anao si haba watamshauri apokee hizo kesi, nina imani ni ugeni kwenye urais . Mfano ambao nimempenda, kea miezi hii mitatu ameacha kuitumia maneno ( mtalitazama, sijui mtafanyaje, mtaamua nk.) Ameanza kuitumia ninawaagiza, nwatakeni fanya hivi, .Hii ndio kauli ya rais kureflect mamlaka aliyonayo, kule mwanzo alikuwa analalamikia mifumo kama sisi raia wa kawaida. Na kwa vile ni msomaji wa social media amebadilika kama tulivyomuomba anaamuru, . Nina imani kubwa kea Samia ,ana international exposure kubwa, atatuvusha akiwa na mchumi binges Mpango kama mshauri mkuu na Majaliwa kama msimamizi mkuu lengo kuu la hayati JPM,(RIP.) litazibika.
Kwanza, rais kasemaje?

Tuhakiki maneno aliyosema kwanza.
 
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
”Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. ” Sio maneno yangu.
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
 
Kifungu 25 (1) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma za mwaka 2002 kinasema..." where a public servant or the disciplinary authority is aggrieved with the decision of the Commission (tume ya utumishi wa umma) SHALL appeal to the President whose decision shall be final".
I thought so.

Maneno halisi aliyosema rais yako wapi?
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
Hayuko sahihi kabisaaa!!!

Kwasababu sheria inasema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana wajibu wa kusikiliza Rufaa zoote na kuzitolea maamuzi yenye haki.
 
Hayuko sahihi kabisaaa!!!

Kwasababu sheria inasema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana wajibu wa kusikiliza Rufaa zoote na kuzitolea maamuzi yenye haki.
Maneno verbatim aliyosema yako wapi?
 
Kwa kiasi gani unaijua Tume ya Utumishi wa Umma??
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
Unaijua Tume ya Utumishi wa Umma??
Ushawahi kupeleka rufaa yako pale??
Kama ulionewa (Kabla ya tamko hili la Rais) ulikata rufaa kwa Mh. Rais kupinga uamuzi wa Tume? Je, kama Tume ilikuonea Ulishinda rufaa yako Kwa Mh. Rais??

Tuanzie hapa kwanza
 
Bado tuendelee kuwasisitizia watu ambao hamtaki kuelewa hata sijui mtu awaambieje!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufanya mambo nje ya watu na vyombo vinavyomzunguka. Sasa mnataka Rais afanye maamuzi gani tofauti na yale aliyoshauriwa na vyombo vilivyopo kikatiba ili vimshauri?

Halafu, uzi huu unadhihirisha inconsistencies katika kufikiri kwa baadhi ya watu. Rais JPM alipigwa sana mawe kwa sababu sometimes alijiongeza nje ya kile alichokuwa akishauriwa na wanaomzunguka. Nyie mliona hafai kwa haiba yake hiyo mkamwita dikteta. Mama Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
Nakubaliana na ww mkuu kuwa Rais anafauata taratibu... Lakini kama kuna mwanya wa kukata rufaa ina maana tume ya utumishi imeonekana kuna muda inaweza kufanya maamuzi ambayo sio sahihi sasa unaposema kuwa kesi ikishaamuliwa kule isifike kwake tena inatoa nafasi kwa waajiri na watuimishi wa tume kufanya maamuzi kwa manufaa yao maana wanajua maamuzi yao hata ukiyakatia rufaa hayatabadilishwa! Kikubwa kama ni hivyo ajitahidi kuweka watu wenye weledi basi kuliko hawa ambao kutwa wanalalamikiwa kuwabeba waajiri na hakutakiwa kuyaongea yale mbele za watu... Nipo kusahihishwa
 
waOhoooo kwani nchi haina Labour Court?au commission ya usuluhishi?kama hatuna ni muhimu tuwe na taasisi hizi mbili na kwa president sio jukumu lake kabisa

Labour court kwa mashauri ya watumishi wa Umma hufuata baada ua uamuzi wa Rais dhidi ya Maamuzi ya Tume. Halafu baada ya mabadiliko ya Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 watumishi wa umma, hawahudumiwi na CMA tena.
 
Bado tuendelee kuwasisitizia watu ambao hamtaki kuelewa hata sijui mtu awaambieje!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufanya mambo nje ya watu na vyombo vinavyomzunguka. Sasa mnataka Rais afanye maamuzi gani tofauti na yale aliyoshauriwa na vyombo vilivyopo kikatiba ili vimshauri?

Halafu, uzi huu unadhihirisha inconsistencies katika kufikiri kwa baadhi ya watu. Rais JPM alipigwa sana mawe kwa sababu sometimes alijiongeza nje ya kile alichokuwa akishauriwa na wanaomzunguka. Nyie mliona hafai kwa haiba yake hiyo mkamwita dikteta. Mama Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
magufuli tunakubaliana kuna mazuri amefanya ila tu mabaya ni mengi mno na mazito. elewa hilo kwanza.
Pili , hebu eleza mwisho wa kesi za utumishi katika mhusika kutafuta haki ni wapi? tuanzie hapo
 
Kama hawamuumizi kichwa anakuja mwz kufanya nn.anajua umuhimu wa mwz sana
Jinga wewe, kwani Mwanza ipo Uganda???! Ivi unadhani kwa Tanzania Rais anategemea kura za kwenye sanduku ili ashinde, Tena mkizingua na mkong'oto tutawapa na kura Mwanza mtatupa kwa 100%
 
Rais anayo mamlaka ya kusikiliza rufaa yoyote ile hata kama imetoka court of appeal... Ndio maana anawasaidizi. Na katiba imempa mamlaka ya kusamehe mtu kama ametiwa hatiani na mahakama. Rufaa au malalamiko yanaruhusiwa kupelekwa kwa Rais. Labda itokee rufaa ni ya kitoto.. ndio maana ilitolewa mfano mtu hajaonekana kazini wiki mbili bila taarifa kisha unakata rufaa kwa Rais inakuwa unapoteza muda.
 
Aifanyie amendment public service act maana Hilo ni takwa la kisheria maana kwa watumishi wa Uma maamuzi ya Rais ndio Final, baada ya hapo mtumishi anatakiwa kwenda mahakama kuu akitaka. Kwa judicial writs.

Ama la afanye amendment ili watumushi wa uma wote waende CMA.
 
Kisheria, rufaa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma inapelekwa kwa Mhe. Rais. Kwa kuwa watumishi wataendelea kufuata sheria, rufaa zitaendelea kupelekwa kwa Mhe. Rais. Labda kama rufaa husika 'hazitafika' au kufanikiwa ziendako.
Fanyeni kwamujib washeria yoote hayo yarufaa na nk hayatatokea
 
Yuko sahihi kabisa , Hilo sio jukumu lake , labda kiundwe chombo kingine Cha kusikiliza ,au iende mahakani, huo ndo mfumo,
Tuna watumishi wangapi wenye kesi, wote waende kwa rais!
Ataweza kuwaamua wote?
Rais ni Taasisi wala siyo mtu. Sheria za kazi ni fani inayosomewa chuoni au katika LLB, au HR au Industrial Relations.

Kwenye kifungu 25 (1) (d) ya Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya 2002, wanaposema Mfanyakazi ambaye hakuridhika naaamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma atakata Rufaa kwa Rais, maana yake Rais ndiye mamlaka. Lakini Rais ana Ofisi yake ya Katibu Mkuu Kiongozi ambayo ina wataalamu wote wa nyanja ambazo Rais anahitahi ushauri.

Baada ya barua kupokelewa, wataalamu wa Ofisi ya KMK wataipitia rufaa, watatafuta kumbukumbu kwa Mwajiri na Tume ya Utumishi na kuchanganua.

Kisha watatoa hitimisho/ pendekezo ambalo ndilo Rais atalisoma na kuandika "Nakubali" au "Sikubali".

Rais kimsingi kama binafsi hafanyi kazi ya kuchambua bali ni timu iliyo ofsini kwa KMK
 
Kama Samia anaona Uraisi ni Mgumu basi kwa heshima na taadhima aachie kijiti mwaka 2025, Lakini kiukweli kabsia na kwa mujibu wa katiba yeye ni mkuu wa utumishi wa Umma nchini na anapaswa kuwasikiliza watumishi. AACHE UVIVU!
 
Bila katiba mpya tutapata shida haswa kwa hawa watawala wa CCM, dawa yao ni kuwaendea kwa waganga wa kienyeji mnamalizana bila lawama.

Sasa Naanza Kuelewa Umuhimu wa katiba Mpya....
Mwanzo sikuona Umuhimu kwasababu Niliona Hata Katiba Mpya Ikiwepo Na Aliekuwepo asipoitekeleza nani atamfanya nini?
Haya yalikuwa Mawazo yangu!
Kwamba Unaweza kuwa na Katiba Mpya na Kama Haifuatwi?
Yaani unaweza kuwa na Katiba ya sasa na Haifuatwi sasa utadai Mpya ili iweje?
Huu ni Mfano tuu!
PIA Nadhani Tume haiko independent,Inaogopa Gharama kama Mtumishi Ana Haki...Yaani Kurejeshewa stahiki zake...
Wanaona hiyo hasara italipa Serikali,Na Serikali inawakilishwa na Tume!
Soma Paragraph hii ya Mwisho Utaelewa ndio kwenye ujumbe Mzito kwanini Tume inaogopa/
Sababu ni Part and Parcel ya Serikali Yaani Kuna Link kati ya Utumishi na Tume!
Mfano Kenye Judge yuko Independent uneona Juzi Jaji Mkuu Mwanamke kamuonya Kenyatta Kuchagua Majaji waliobaki kwa Mujibu wa Katiba!
Hapa Kwetu Vyombo hivyo Haviko Independent 100%
 
Back
Top Bottom