Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
Kwani mahakama hazitoi haki? Au inakatazwa mtumishi kupeleka mashtaka kortini ili kudai haki yake iliyoporwa?
Ikiwa Rais atafanya kazi zote basi hatuna haja ya kuwa na mahakama wala idara zingine...
Hivi kwanini hatujui njia zenye afya kwa kudai haki zetu badala yake tunataka wanasiasa ndio watatue matatizo? Au ndivyo tulivyolelewa?
Haki haiombwi...
 
Katika hili Rais Samia anakosea, Yeye ndiye mkuu wa utumishi wa umma nchini, haifai hata kidogo kujivua wajibu wa kuhakikisha haki ya mtumishi inatendeka nchini.

Kauli yake hii ni kukwepa majukumu ya rais. Huu ni msiba mkubwa sana!
 
Kifungu 25 ( 1) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 ikisomwa pamoja na na Sheria ya marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na 28 ya mwaka 2007, inamtambua Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kama ndiye Mkuu wa Watumishi wote nchini na ndiye Mamlaka ya Rufaa kwa wafanyakazi ambao hawajaridhishwa na maamuzi ya Tume ya Utumishi ya Umma.

Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 kifungu 2 (f) na 60 (5) nazo zinakazia majukumu ya Rais kwa Rufaa za Wafanyakazi.

Hivyo kama kauli hiyo ya mtoa mada ni ya kweli, basi Rais atakuwa ameshauriwa vibaya. Na kwa mintaarafu hiyo atakuwa anakana kutekeleza majukumu yake yanayotambuliwa kisheria.
 
Watanzania tunapenda Sana kunyongana na kukandamizana kwenye haki anayostahili mwingine, kisa tu mtu Fulani Yuko juu Kwa kipindi hiko

Huko kunaitwa, ni kujisahaulisha Kwa maksudi ulikotoka, ukipandishwa na Mungu, unasahau ulikotokea, unaanza kuamua unavyojiskia badala ya kumpa heshima huyo Mungu aliyekupandisha kukupa nafasi hiyo,

Ukipewa nafasi ya juu, si kwamba umepewa sehemu ya kuwanyonga wengine, no, ni kuwalinda na kuwatetea popote pale

Na ndiyo maana tunajikita umepoteza kazi zetu Kwa haraka Sana ama kupoteza uhai kabisa Kwa sababu ya dhuluma ambazo Mungu anayetuamini si wa kuvumilia Sana mateso ya wengi Kwa ajili ya mmoja tu anayejiona yeye ndio kafika na asijue kwamba, Mungu yeye ni Mungu wa majeshi, maana yake anao watu mahiri na wazuri mno kuliko mmoja tu unayenyima haki za watu wake, Tutendeani mema ndugu zangu
 
Ndiyo Mkuu
Basi huyo rais ni mjinga, mvivu na anapingana na utawala wa sheria.

Yani kuna kazi ambayo kisheria inatakiwa kufanywa na rais, halafu yeye anaikataa.

This is a case of dereliction of duties. Rais kakataa kazi yake.

Basically, abdication.

What's next? Atakataa kupitia na kusaini miswada iwe sheria?

Anakataa kazi, lakini privileges za urais anazikubali.

Ningemuelewa kama angesema atajipanga kuweka mchujo mkali hapo ofisi ya rais, ili kuchuja rufaa zisizo na merit. Angeweza ku delegate mchujo huo kwa watu maalum Ikulu. Maana si lazima afanye yeye binafsi mchujo, anaweza kuagiza mchujo mkali ofisini kwake. Urais ni taasisi.

Yeye personally akapata kesi chache tu zenye merit.

Maana inawezekana rais akasumbuliwa na lundo la kesi zisizo na merit pia, na yeye ana kazi nyingi.

Lakini yeye kakataa kabisa kusikiliza kesi kama vile yeye si rais.

Rais kachemka.
 
Bila katiba mpya tutapata shida haswa kwa hawa watawala wa CCM, dawa yao ni kuwaendea kwa waganga wa kienyeji mnamalizana bila lawama.
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Bado tuendelee kuwasisitizia watu ambao hamtaki kuelewa hata sijui mtu awaambieje!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufanya mambo nje ya watu na vyombo vinavyomzunguka. Sasa mnataka Rais afanye maamuzi gani tofauti na yale aliyoshauriwa na vyombo vilivyopo kikatiba ili vimshauri?

Halafu, uzi huu unadhihirisha inconsistencies katika kufikiri kwa baadhi ya watu. Rais JPM alipigwa sana mawe kwa sababu sometimes alijiongeza nje ya kile alichokuwa akishauriwa na wanaomzunguka. Nyie mliona hafai kwa haiba yake hiyo mkamwita dikteta. Mama Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
Kitu cha msingi kabisa hapa ni kwamba Rais Hassan kakataa kazi yake ambayo anatakiwa kufanya kisheria.

Amekuwa kama housegirl ambaye mkataba wa kazi unasema atafanya usafi nyumba nzima, halafu yeye anasema hatafagia chooni.

Kama hataki kufanya kazi yake, ambayo alitakiwa kuijua kabla ya kuikubali, basi ajiuzulu wengine watafanya.
 
Kwani mahakama hazitoi haki? Au inakatazwa mtumishi kupeleka mashtaka kortini ili kudai haki yake iliyoporwa?
Ikiwa Rais atafanya kazi zote basi hatuna haja ya kuwa na mahakama wala idara zingine...
Hivi kwanini hatujui njia zenye afya kwa kudai haki zetu badala yake tunataka wanasiasa ndio watatue matatizo? Au ndivyo tulivyolelewa?
Haki haiombwi...
Rais hatakiwi kufanya kazi zote.

Rais anatakiwa kusikiliza rufaa.

Tena wala hatakiwi kusikiliza rufaa zote.

Anaweza kuweka mchujo mkali ofisini kwake, wasaidizi wake wakafanya mchujo. Akatupilia mbali rufaa nyingi kwamba hazina merit, akasikiliza rufaa hata moja tu kwa mwezi.

Lakini, hata kufanya hivyo kakataa.

Maana yake, kuna mtu ataonewa, atashindwa kukata rufaa kwa rais.

Kwa sababu rais kakataa kufanya kazi yake ya kusikiliza rufaa.
 
Rais hatakiwi kufanya kazi zote.

Rais anatakiwa kusikiliza rufaa.

Tena wala hatakiwi kusikiliza rufaa zote.

Anaweza kuweka mchujo mkali ofisini kwake, wasaidizi wake wakafanya mchujo. Akatupilia mbali rufaa nyingi kwamba hazina merit, akasikiliza rufaa hata moja tu kwa mwaka.

Lakini, hata kufanya hivyo kakataa.

Maana yake, kuna mtu ataonewa, atashindwa kukata rufaa kwa rais.

Kwa sababu rais kakataa kufanya kazi yake ya kusikiliza rufaa.
Mkuu "buruta" mahakamani mpaka haki ipatikane..
 
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
Lakini pia anasahau kuwa muundo wa utumishi kuweka mamlaka ya Rais kuwa ndio ngazi ya mwisho ya rufaa juu ya mambo yote yahusuyo utumishi wa umma iko kisheria vinginevyo isingewekwa.
 
Rais hatakiwi kufanya kazi zote.

Rais anatakiwa kusikiliza rufaa.

Tena wala hatakiwi kusikiliza rufaa zote.

Anaweza kuweka mchujo mkali ofisini kwake, wasaidizi wake wakafanya mchujo. Akatupilia mbali rufaa nyingi kwamba hazina merit, akasikiliza rufaa hata moja tu kwa mwezi.

Lakini, hata kufanya hivyo kakataa.

Maana yake, kuna mtu ataonewa, atashindwa kukata rufaa kwa rais.

Kwa sababu rais kakataa kufanya kazi yake ya kusikiliza rufaa.
KAMA NI HIVYO ATOKE OFISINI AWAACHIE AMBAO WAPO TAYARI KUWATUMIKIA WATANZANIA.
 
Mkuu "buruta" mahakamani mpaka haki ipatikane..
Sheria inasema watumishi wana haki ya kukata rufaa kwa rais.

Rais akikataa kusikikiza rufaa za watumishi, amewanyima haki.

Sasa ukisema "buruta mahakamani mpaka haki ipatikane" wakati mchakato wa kupata haki unaruhusu rufaa kwa rais, unajichanganya.

Unanikumbusha msemo mmoja wa kabaila wa Marekani Henry Ford.

Henry Fird alikuwa na kiwanda cha magari Ford. Alitengeneza magari akauza kwa bei rahisi.

Tatizo lake magari yake yote meusi. Hayana rangi nyingine.

Watu wakawa wanamuuliza, tunaweza kupata magari ya rangi yoyote tunayotaka?

Akawajibu, mnaweza kupata rangi yoyote mnayotaka, ikiwa rangi mnayotaka ni nyeusi.

Sasa na wewe hapa umekuja na habari kama za Henry Ford.

Unataka watu wapate haki, ikiwa tu haki inatoka mahakamani.

Kuna mchakato unaoruhusu rufaa kwa rais.
 
Kitu cha msingi kabisa hapa ni kwamba Rais Hassan kakataa kazi yake ambayo anatakiwa kufanya kisheria.

Amekuwa kama housegirl ambaye mkataba wa kazi unasema atafanya usafi nyumba nzima, halafu yeye anasema hatafagia chooni.

Kama hataki kufanya kazi yake, ambayo alitakiwa kuijua kabla ya kuikubali, basi ajiuzulu wengine watafanya.
Tatizo moa mada ameileta mada kwa kukidhi mahitaji yake, au amesimuliwa tu hakusikia rais alichoongea.
Rais alisema hivi, nimewateua mkafanye kazi mlizopangiwa, sio unaacha kufanya kazi haupo kazini wiki mbili unafanya mambo yako binafsi na ukichukuliwa hatua unakimbilia kukuta rufaa kwa rais. Hapo ndipo akatoa tamko rufaa kama hizo hazitaki. Hakusema rufaa zote hazitki. Si mwandishi nzuri nazani umenielewa ie amemaanisha kuna watu wanakutwa na makosa ila wanakata rufaa kwa kutegemea wanajuana na kiongozi wa juu hivyo rufaa itaamliwa kwa upendeleo
 
Kwani sheria inasemaje?

Kisheria watu wanaruhusiwa kukata rufaa kwa rais?
Kifungu 25 (1) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma za mwaka 2002 kinasema..." where a public servant or the disciplinary authority is aggrieved with the decision of the Commission (tume ya utumishi wa umma) SHALL appeal to the President whose decision shall be final".
 
Mama anakimbia majukumu yake.
Kisheria, rufaa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma inapelekwa kwa Mhe. Rais. Kwa kuwa watumishi wataendelea kufuata sheria, rufaa zitaendelea kupelekwa kwa Mhe. Rais. Labda kama rufaa husika 'hazitafika' au kufanikiwa ziendako.
 
KAMA NI HIVYO ATOKE OFISINI AWAACHIE AMBAO WAPO TAYARI KUWATUMIKIA WATANZANIA.
Kuna binti mmoja tulikuwa naye hapa JF.

AlIkuwa mwanaharakati mzuri wa CHADEMA.

Akagombea ubunge.

Akaukosa. Sijui kama kura hazikutosha au aliibiwa na CCM.Ila alilalamika kaibiwa, CCM nao wakavutia ngozi kwao.

Basi, CHADEMA wakamfanyia mpango wa kupata ubunge kwa viti maalum kutika katika chama.

Akapata ubunge.

Kupata ubunge sasa. Vikao kadhaa vya bunge, akaanza kulalamika.

Bunge liko boring. Yeye kazoea uanaharakati. Alikuwa hajqaua kuwa bunge lina kazi kubwa ya kujifunza sheria, kanuni, kusoma miswada, kujielimisha mengi.

Akawa analalamika kwamba bunge liko boring.

Nikasikitika sana. Kwa sababu niliona wazi mfano wa mtu anayetaka power for the thrill of having power, halafu akiipata hajui kuitumia, hana ambition, hajui rules of power.

Rule moja ya power ni kwamba, power ni kama msuli, usipoutumia msuli, unasinyaa.

Rais Samia ana power ya kusikiliza rufaa. Yani hata kuikubali symbolic tu kungetisha.

Alichofanya ni ku undermine power yake.

Kwa sababu, sasa hivi ikitokea mtu kaonewa na rais anataka kumsaidia kwa kusikiliza rufaa, kufanya hivyo kutafanya rais aonekane kigeugeu.

Rais anaonekana kama amekuwa rais kwa bahati mbaya bila kuelewa na kukubali kazi za urais ni nini.

Rais kala kiapo cha kuitetea katiba, katiba inasema nchi iongozwe kwa utawala wa sheria, sheria inasema rais asikilize rufaa, rais anasema hasikilizi rufaa.

Rais kavunja sheria, kavunja kiapo, kavunja katiba.

Amenikumbusha yule binti wa CHADEMA aliyeingia bungeni bila kujua kazi za mbunge ni zipi, halafu muda mfupi baadaye akasema bunge liko boring.
 
Tatizo moa mada ameileta mada kwa kukidhi mahitaji yake, au amesimuliwa tu hakusikia rais alichoongea.
Rais alisema hivi, nimewateua mkafanye kazi mlizopangiwa, sio unaacha kufanya kazi haupo kazini wiki mbili unafanya mambo yako binafsi na ukichukuliwa hatua unakimbilia kukuta rufaa kwa rais. Hapo ndipo akatoa tamko rufaa kama hizo hazitaki. Hakusema rufaa zote hazitki. Si mwandishi nzuri nazani umenielewa ie amemaanisha kuna watu wanakutwa na makosa ila wanakata rufaa kwa kutegemea wanajuana na kiongozi wa juu hivyo rufaa itaamliwa kwa upendeleo
Kaa minajili hiyo, namuunga mkono rais.

Rais anatakiwa kuulinda muda wake.

Akitaka kusikiliza kila rufaa ya kijinga atapoteza muda mwingi sana.

Ndiyo maana hapo juu nilisema, nitamuelewa kama akiweka chujio kuchuja rufaa zisizo na merit, asikiki,e chache zenye merit.

Watanzania wengi wana tatizo la kusoma na kusikikiza kwa ufahamu.

Pia, wengine wengi wanapotosha makusudi kisiasa.
 
Kwa sababu kuna utata juu ya kilichosemwa.

Na kwa sababu tunataka kuondokana na upotoshwaji wa kisiasa.

Kuna mtu anaweza kuweka maneno halisi, kwa muktadha halisi, ikiwezekana video, tuone alichosema rais neno kwa neno?

Ikiwezekana video itakuwa vizuri zaidi, ila hata audio au direct quote yenye reputable source itakubalika.
 
Kama sheria inasema rufaa iende kwa rais , hakuna jinsi mama azipokee na azitolee maamuzi. There is no way mhe. Mama Rais wa JMT akwepe utekelezaji wa sheria iliyotungwa na bunge,itakuwa ni ukiukwaji wa katiba. Ninajiuliza kama marais walipoita wangesoma mahakama ikishahukumu mtu anyongwe , msilete faili mezani kwangu kusubiri msamaha wa rais,ni wananchi wengi wangeishanyongwa. Lakini sheria ilitungwa vile wakijua rais kama binadamu anaweza akamhurumia mkosaji. Lakini kubwa zaidi kesi ya mtumishi wa umma dhidi ya mwajiri ni ya watu wawili ambapo mwajiri ni mwenyenacho na mtumishi asiyekuwa nacho . Matokeo ni kuwa mtumishi ataminywa tu . Duniani inasadikiwa ni 3 asilimia ya binadamu hawawezi kula rushwa na kupindisha sheria majaji wakiwemo. Rais asikwepe kupokea na kutoa misamaha akijridhisha mnyonge akionewa .Kwanza uongozi bora ni pale ubinadamu unapotumika kupendelea mnyonge kuliko uache sheia ichukue mkondo, mwanasiasa mahiri kama Samia asijinyime fursa ya kusomesha ubinadamu wake. Akikaa na na washauri wake ambao anao si haba watamshauri apokee hizo kesi, nina imani ni ugeni kwenye urais . Mfano ambao nimempenda, kea miezi hii mitatu ameacha kutumia maneno ( mtalitazama, sijui mtafanyaje, mtaamua nk.) Ameanza kutumia ,ninawaagiza, nawatakeni fanyeni hivi, .Hii ndio kauli ya rais kureflect mamlaka aliyonayo, kule mwanzo alikuwa analalamikia mifumo kama sisi raia wa kawaida. Na kwa vile ni msomaji wa social media amebadilika kama tulivyomuomba anaamuru, . Nina imani kubwa kwa Samia ,ana international exposure kubwa, atatuvusha akiwa na mchumi bingwa Mpango kama mshauri mkuu na Majaliwa kama msimamizi mkuu lengo kuu la hayati JPM,(RIP.) litazibika.
 
Back
Top Bottom