Rais Samia Kiwanda cha Chibuku/ Darbrew LTD kilifungwa tangu mwaka 2018. Muwekezaji yupo lakini Watendaji wa Jiji la Ilala wanakwamisha

Katika pombe ambazo ni icon ya Dar es Salaam basi Chibuku ni namba yoja. Kumbe kuna mashetani wamefanya hujuma mbaya namna hii kwa faida tu ya matumbo yao! Hivi waafrika tuna laana gani jamani! Hii pombe ilitakiwa ifanyiwa promotion ili ienee Tanzania nzima na watu waache kunywa pombe hatarishi huko mitaani. Nakumbuka miaka ya nyuma Chibuku ilikuwa inanywewa na watu wa maana kweli kwani ni pombe moja nzuri sana. I hapo mamlaka zitafanyia kazi haya malalamiko yenu ambayo kimsingi ni wazalendo wote.
 
Asante,tayari kinywaji hiki kilianza kunyweka hadi ushuani kama Masaki na Mbezi beach. Mkoani kilifika pia kama mwambao wa pwani yote ya bahari hadi Mtwara na kilikubalika sana,pia Morogoro.
 
Chibuku ni lishe pia,na ilisaidia sana watu kuepuka aina ya vinywaji unavyozungumzia, sokoni tunaingia very soon mkuu. Tusaidiane tu kusambaza taarifa hizi za hujuma zifike kwa wakubwa kwa maamuzi
Ni kweli mkuu, mi mwenyewe nilikuwa mteja mzuri sana wa chibubu ile take away.
Ile unapiga 2 in 1, yaani unalewa na kupata lishe kwa wakati mmoja.
 
Kinachoimaliza hii Nchi ni tamaa,sasa angalia wanataka kukiua kiburudisho cha Watu wa Dar
 
Nchi ngumu sana hii! Watu hawana kabisa uzalendo!
 
Chibuku ni lishe pia,na ilisaidia sana watu kuepuka aina ya vinywaji unavyozungumzia, sokoni tunaingia very soon mkuu. Tusaidiane tu kusambaza taarifa hizi za hujuma zifike kwa wakubwa kwa maamuzi
Ni kweli chibuku inanenepesha hadi kitambi fulani hivi cha kizushi lazima kikutoke
 
Serikali ya awamu ya Tano halikuliona hili na kulifanyia kazi?
TBL wamehonga sana na wanaendelea kuhonga kudhibiti informations, Makonda alipokuwa RC wateja walimfuata kulalamika kusitishwa kwa uzalishaji,nadhani TBL walimuwahi na akapata ganzi maana alikuwa kimya wala hakufuatilia tena licha ya ahadi alizotoa,RC Kunenge alilifanyia kazi sana na kubaini uzembe mkubwa wenye mianya ya rushwa. Aliagiza ufanyike uwekezaji haraka ndani ya wiki mbili apewe huyo muwekezaji,alipohamishwa tu wadau wakazuia
 
Kwa sasa hilo eneo nadhani ni depot ya TBL kama sijakosea .Hiyo ishu Prof: Kitila anatakiwa ndio aipatie ufumbuzi hata bila kumhusisha mama ,maana yeye ndio waziri husika na pia ndio mbunge wa jimbo la Ubungo.
 
Aisee chibuku!Mmenikumbusha mbali sana!
 
Kwa sasa hilo eneo nadhani ni depot ya TBL kama sijakosea .Hiyo ishu Prof: Kitila anatakiwa ndio aipatie ufumbuzi hata bila kumhusisha mama ,maana yeye ndio waziri husika na pia ndio mbunge wa jimbo la Ubungo.
Sio depot ni kiwanda mkuu,tatizo Prof Kitila analijua lakini hatujui kwa nini halifanyii kazi maana sio uwekezaji mpya kwamba unahitaji muda sana, DarBrew Ltd ipo tangu 1967 kinachotakiwa ni muwekezaji mpya tu ila danadana zimezidi ndio maana ni bora mama xajue sasa akina nani wanamkwamisha kupata kodi. Three years of waiting for an investor(and he was there before and they know him) to be accepted!...it's a big joke.
Environment isn't friendly to investors at all !
 
TBL ilipata management ya kihuni walinunu hisa Darbrew lakini strategically wao walikuwa hawataki kuzalisha bali walikuwa wanalitaka like eneo la kiwanda.

Hata Konyagi nayo inasuasua TBL hataki kuweka mtaji wa maana amengangania ku import beverages kageuka dalali. Hii ilipelekea wao TBL kuuza hisa zao kwa Ab Inbev maarufu kama Budweiser producer. Ambao nao hawana priority ya kuzalisha vitu kama konyagi na chibuku.

Hii suala si la mama ni la waziri wa Viwanda na waziri wa ardhi warudishe ile ardhi kwa Darbrew then investor apewe full asset. Halafu kuna watanzania wahuni wapo kwenye hizo management badala ya kueleza ukweli hao wazungu wao wanawaza bonus mwisho wa mwaka. Dada yetu tunajua hukuwa hapo muda lakini una impact sana kwa wawekezaji wa TBL G. Mutagwahya hebu washauri vizuri nchi inufaike kwa viwanda. Dar brew itatoa ajira na kuuza chibuku.

Kuna wakati tunamkumbuka Nyerere kwa sababu ya akili,misimamo na ufuatiliaji. Hivi asingekuwa Nyerere leo SGR, au Tazara zingekuwa na eneo kweli si lingekuwa lishauzwa kama ilivyouzwa Tanganyika Packers.
 
Asante sana kwa mchango wako uliotukuka,umeongea ukweli uliopo,kwa pamoja tutaokoa ajira za watu,mali ya umma na kuisaidia serikali kupata mapato.
Lakini waziri wa viwanda Prof. Kitila ni mbunge wa eneo kilipo kiwanda na aliahidi kwenye kampeni tena kupitia ITV kuwa angelimaliza hili suala mara moja lakini kiukweli hatujaona msaada wowote kutoka kwake na taarifa anayo. Sasa hatujui kwa nini ametupuuza,ila uwa anaongea sana na watu wa TBL.
Mpaka tunataka mama aingilie kati tume hustle sana uku kwa wasaidizi wake, eg. waziri wa zamani wa TAMISEMI mh. Jaffo anajua habari hii alionekana kuwa kigugumizi pia wakati anajua suala lilivyo.
 
Naamini bado watakua wanahitaji sana mana zile buyu zilikua na ujazo mwingi watu wakazipenda sana.
 
Mkirudi mtakuta kizazi cha wanywa chibuku wamehamia kwenye double kick wanatetemeka tu mikono na midomo kama wagonjwa wa matenguchi.
Watumiaji wa chibuku wanakunywa banana na wanzuki mambo yakiwa magumu
 
Chibuku pombe na lishe tosha, mana vitu vanachanganya kule hatari.
 
Watumiaji wa chibuku wanakunywa banana na wanzuki mambo yakiwa magumu
Huku niliko wanakunywa hadi pombe ya mtama na komoni. Ila mimi komoni ya Dar ilinishinda sio nzuri kama ya Iringa Mbeya na Njombe. Ile unakunywa halafu unatoa gesi puani.
 
Michakato itatuletea majanga.waziri wa Tamsem .waziri wa uwekezaji biashara na viwanda.wapo watanzania waliokuwa wanauza mahindi na mtama leo wanalia mapato ya serikali yanapotea kulikoni?wanaolalamika ni wafanyakazi this can be economic sabotage. Wahusika bila kigugumizi tekeleza wajibu wenu kwa mstakabali mzima wa taiga let.
 
Mi sikuelewaga kwanini kilikufa...kumbe hujuma
 
Nakumbuka takwimu za Chibuku kuwa mlipa kodi mkubwa. Nilikuwa nashangaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…