Vonzelewsk
Member
- Sep 20, 2018
- 93
- 283
DAR ES SALAAM — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kihistoria nchini Russia kuanzia Juni 3 hadi 5, 2026, kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ziara hiyo itakuwa ya pili kufanywa na Rais wa Tanzania nchini Urusi tangu Hayati Julius Kambarage Nyerere alipozuru taifa hilo mwaka 1969, takribani miaka 57 iliyopita.
Wakati wa ziara hiyo, Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na Rais Putin kuhusu kuimarisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, elimu, sayansi na teknolojia, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.
Aidha, Rais Samia atashiriki na kuhutubia Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026), moja ya majukwaa makubwa duniani yanayowakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, taasisi za kifedha na wadau wa sekta binafsi kujadili masuala ya uchumi na maendeleo.
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu