Rais Samia kufanya ziara nchini Urusi kuanzia Juni 3 hadi Juni 5, 2026

Rais Samia kufanya ziara nchini Urusi kuanzia Juni 3 hadi Juni 5, 2026

Naona kaamua kuwatumia ujumbe kina Cruz na Trump wapitishe na kusaini ule muswada kuhusu Tanzania haraka.
Ndiyo basi tena tunaenda kuwa Zimbabwe nyingine.

Ziku za Mwisho za kufa Zimbabwe Mugabe alikwenda sana Russia
Ya mwisho alikwenda 2015

Western wakikukazia siyo Russia wala china watakaokusaidia
 
Russia na china siyo wa kuwategemea wao wenyewe bado wanajitafuta ..western ndio wenye dunia yao wakikkukataa utoboi
China anajitafuta? Hamna mkuu haya majamaa yameshajipata. Huoni ziara za viongozi wa magharibi kumfata Xi wayajenge? Sema mama awe tu makini humo njiani kuna drone za Ukraine zinaongozwa na wahuni waliochanganywa na vita zinagonga chochote muda wowote
 
DAR ES SALAAM — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kihistoria nchini Russia kuanzia Juni 3 hadi 5, 2026, kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ziara hiyo itakuwa ya pili kufanywa na Rais wa Tanzania nchini Urusi tangu Hayati Julius Kambarage Nyerere alipozuru taifa hilo mwaka 1969, takribani miaka 57 iliyopita.

Wakati wa ziara hiyo, Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na Rais Putin kuhusu kuimarisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, elimu, sayansi na teknolojia, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.

Aidha, Rais Samia atashiriki na kuhutubia Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026), moja ya majukwaa makubwa duniani yanayowakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, taasisi za kifedha na wadau wa sekta binafsi kujadili masuala ya uchumi na maendeleo.

Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

View attachment 3599431
Tunaomba abaki huko huko tafadhali
 
China anajitafuta? Hamna mkuu haya majamaa yameshajipata. Huoni ziara za viongozi wa magharibi kumfata Xi wayajenge? Sema mama awe tu makini humo njiani kuna drone za Ukraine zinaongozwa na wahuni waliochanganywa na vita zinagonga chochote muda wowote
Kujipata kwa kiwango cha kumzuia USA na Ulaya wasifanye jambo lao la kiuchumi kwa nchi ndogo wakitaka kulifanya nadhani bado. Ila kujipata yeye kama yeye tayari maana si nchi ambayo USA au Ulaya wanaweza kuipelekesha kiuchumi. Ila kusema USA, Ulaya wawe maadui wa kiuchumi na mlinzi awe China sidhani kama anaweza kukuhakikishia ulinzi wa kiuchumi.
 
My Take
Sio Kila Rais wa Tanzania anaweza Kualikwa Nchini Urusi,hii huja Kwa mtu kwenye msimamo na asiyeyumbishwa na aliyekataa kuwa kibaraka wa beberu wa West wanaowafashili wale vibaraka wanaojiita Wapinzani.

Hii sio tuu kwamba ni Heshima binafsi Kwa Rais Samia Bali ni Heshima Kwa Nchi kwamba imeendelea kusimamia msimamo wake usioyumba.

Haters wa SSH kazi wanayo.

View: https://www.instagram.com/p/DZDVVrrs6aQ/?igsh=MWZncTF0anFhYTN3Mg==
 
Fazafaka hawezi kupata mwaliko kutoka nchi zinazoendesha mambo yake kwa kufuata the rule of law. Other than invitations from fellow African dictators, ataendelea kupata mialiko ya mazafakas wa Russia, China, North Korea, na Uarabuni.

Ameshaishushia nchi yetu hadhi.
Kwa hiyo kwenu nyie ukialikwa na USA na Europe ndo unakuwa na hadhi.
 
Back
Top Bottom