Rais Samia kuhojiwa sana huko Marekani inashusha hadhi yake kama Rais na hadhi yake kama Taifa

Rais Samia kuhojiwa sana huko Marekani inashusha hadhi yake kama Rais na hadhi yake kama Taifa

Kumbuka yeye ni mke wa mtu, mama na bibi wa wajukuu kadhaa....
Muacheni mama afanye na shoping kwaajili ya familia na akimaliza aende akabembee kabla hajarudi nyumbani.
Ila kwajirani kuna msiba mzito, sijui atamtuma nani..!!🙄
Acting President atatuwakilisha, sidhani kawa kaiacha nchi kwa wiki mbili nzima bila kukasimu madaraka.
Hii sio Jamhuri ya ndizi.
 
Tunasubiri state visit ya mama huko Britain baada ya hiyo ya US kukamilika kwa kishindo 😉

Heshima hii haipotena sikuhizi mama ni kwenda kuzindua movie na hawezi karibishwa WH kwa hilo... ataishia kuongea na akina Kamala full stop. Huko ni kutema upupu tu...umbea wa ki pwani na vijembe.
 
Wewe ni poyoyo
Mama ndiye sterling kwenye hiyo movie, sasa unataka wahojiwe simba au swala?
Watazamajj wakiambiwa tutakuwa live na Rais aliyetengeneza fialmu ya Royal tour viewership inakuwa juu sana na ndio kuitangaza ili itazamwe na wengi hatimaye lengo la kuitangaza nchi kiutalii lifikiwe

Sasa unataka Msigwa au Abasi wakaizungumzie? Nani anawajua au atajenga interest ya kuwasikiliza?
Kwa taarifa yako TZ haijulikani kiivo huko duniani achilia mbali hao unaotaka waseme.
Watazamaji watavutiwa tu na neno "president"
Mama Samia ni Rais wa JMT lakini sio Wildlife Proffesional.

Ingefaa kama angeambatana na crew iliyosheheni wataaluma wa Wildlife Experts ili kwenye maswali ya kitaaluma wafanye kazi yao ipasavyo.
 
Mama Samia ni Rais wa JMT lakini sio Wildlife Proffesional.

Ingefaa kama angeambatana na crew iliyosheheni wataaluma wa Wildlife Experts ili kwenye maswali ya kitaaluma wafanye kazi yao ipasavyo.
Wataalamu wa wanyama pori sio lazima wawe wanajua kutangaza biashara ya Utalii. Mama anachofanya ni ku-showcase vivutio vya utalii kwa kutumia filamu aliyoshiriki kuitengeneza.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, maana kila ninavyofungua kucheki Royal Tour naona yuko kwenye vyombo vya habari akihojiwa na kujibu

Kuna sehemu sioni kama ni heshima sana kwa Rais kuhojiwa kila mara tena nje ya nchi hali ana crew kubwa tu ambayo anaweza kuitumia kufanya yote hayo.

Au hawaamini hadi yeye mwenyewe ndio ahojiwe lakini kama ambavyo mnajua kuwa kizungu sio lugha yetu inawezekana kabisa akachapia na matokeo yake akafanyika kituko kwenye mitandao ya kijamii ya huko.

Nijuavyo mimi Urais ni nembo kubwa hivyo inalidwa kwa gharama kubwa sana na kuheshimiwa.

MAMA RUDI NYUMBANI INATOSHA SASA. RAHA YA MGENI AKAE SIKU CHACHE SIO HADI WAKUCHOKE
Watanzania hatujui tunachotaka. Miaka yote tunadai Nchi yetu Ina vivutio vingi kuliko nchi nyingi duniani. Hii ni pamoja na Mt Kilimanjaro, Serengeti National Park, Ngorongoro caldera na Stone town ya Zanzibar. Lakini pamoja na vivutio hivyo, nchi yetu haipati mapato ya utalii tunayo stahili kwa kuwa HATUJAJITANGAZA.

Kwa mfano watu wengi duniani huamini kuwa Mlima Kilimanjaro uko Kenya japo unainekana ukiwa Nairobi. Na kwa mantiki hiyo Kenya inapata sana mapato ya utalii kuliko Tanzania.

Hii Royal Your ya Samia ndiyo mkakati mkubwa wa kwanza wenye maana ambao Tanzania inaufanya kwa Dunia toka tupate uhuru kutambulisha vivutio vyetu vya utalii.

Nani kati yetu hapa anafahamu ratiba ya hilo tukio na target audience zaidi ya Peter Greenberg na timu yake? TUNABWAWBWAJA tu

Sasa sielewi tunataka nini maana TUNAPONDA kila ambacho Rais anafanya.
 
Mama Samia ni Rais wa JMT lakini sio Wildlife Proffesional.

Ingefaa kama angeambatana na crew iliyosheheni wataaluma wa Wildlife Experts ili kwenye maswali ya kitaaluma wafanye kazi yao ipasavyo.
Samia hajakwenda kuwinda wanyama New York. Kule anajitaji wataalamu wa marketing, advertising, public relations na film production.
 
Si anajua kizungu kuliko marehemu. Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa. Zaidi ya miaka 6
 
Kumbuka yeye ni mke wa mtu, mama na bibi wa wajukuu kadhaa....
Muacheni mama afanye na shoping kwaajili ya familia na akimaliza aende akabembee kabla hajarudi nyumbani.
Ila kwajirani kuna msiba mzito, sijui atamtuma nani..!![emoji849]

Tena shopping ya Eid eti
 
Back
Top Bottom