Rais Samia kuhutubia na kufungua Bunge la 13, leo Ijumaa Novemba 14, 2025

ni jambo linalosubiriwa kwa hamu na watanzania wote kwa ujumla ni kama mama anakwenda kuliponya taifa ukitizama kwa umakini
Kiongozi umesema kuliponya taifa au nimesoma vibaya?

Unaweza kuponya taifa kwa hotuba ya siku moja kweli?Kwa mfano kuna watoto ni yatima hivi tunavyozungumza wazazi wao wameuliwa siku na baada ya uchaguzi(kwamba kwa hotuba ya leo hii inaweza kurudisha mambo kwenye usawa)

Kuna watu leo hii wako magereza wanapitishwa katika tabu zote na wengi wao walikamatwa hata hawakuwa sehemu ya vurugu zilizotokea(hawa nao wataponywa kwa hotuba ya leo)

Sawa kiongozi ngoja tusubiri uponyaji wa leo
 
Sa100 hataki hata kusubiri Watu wazike Watu wao. Like nothing happened in the country.
Aliwabembeleza sana hao Gen Z, msifanye maandamano, hayo mengine yanazungumzika. Vijana wakakomaza fuvu awafanyaje sasa.
 
ni jambo linalosubiriwa kwa hamu na watanzania wote kwa ujumla ni kama mama anakwenda kuliponya taifa ukitizama kwa umakini
Kumbuka yeye ndiye mwendelezaji wa matatizo ya nchi hii na pia mwasisi wa matatizo mapya. Ataponyaje taifa?
 
Nadhani leo anaweza kuimalizia nchi kuisagasaga baada ya kumeguka vipande vipande au akaregret kwa kilichotokea na kuanza kukusanya vipande vipande vilivyomeguka
 
Ungekuwa wewe nadhani ungewachekea na kuwaimbia mapambio ili wafanye vile wanajisikia.
Ningewakamata. Ningewapiga mabomu ya machozi, maji ya washa washa. Nisingeua watu wanaokimbia, nisingeua watu wapo kwenye magari yao binafsi.

Hii siyo mara ya kwanza maandamano kutokea TZ, watu walikuwa wakikamatwa au kupigwa virungu! Hii ya risasi ni mpya. Ni mauaji ya HALAIKI, haikubaliki.
 
Ulitakiwa uwe Polisi usaidie nchi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…