Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Rais SSH kuingia na mlinzi wa kiume mskitini ni jambo la kawaida kutokana na sababu mbali mbali , hasa kama kuna tishio la usalama au kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokusanyika kwa pamoja.

Tujiepushe na mihemko isiyo na tija na badala yake tufikirie suluhisho zinazojenga na kuheshimu maadili ya jamii husika na kuhakikisha usalama na utulivu wa Rais.

Katika Quran, hakuna aya inayosema moja kwa moja kuwa ni marufuku kwa mwanaume kuingia sehemu ya wanawake msikitini. hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja na mila na desturi za Kiislamu. Kwa mfano, katika hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W), kuna maelekezo yanayohimiza heshima na mipaka baina ya wanaume na wanawake wakati wa ibada ili kuepusha fitna na kudumisha heshima.( kuepusha matamanio ya kimapenzi ndani ya ibada. )

Ibn 'Umar aliripoti kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) alisema, "Usiwazuie wanawake wa Allah kwenda kwenye misikiti ya Allah" (Sahih Muslim, Kitabu 4, Hadithi 891). Hadithi hii inaonyesha kwamba wanawake wanaruhusiwa kwenda msikitini, lakini haina amri maalum kuhusu maeneo maalum ndani ya msikiti. Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.

Katika mazingira ambapo kuna haja ya kuwepo na walinzi wa kiume kwa sababu za kiusalama, ni kwamba tunahakikisha hatua hizi zinachukuliwa kwa njia inayoheshimu mipaka ya kijinsia na dini, kulinda usalama bila kuvuruga utulivu wa ibada.( na hiki ndo amefanya RAIS SSH wa JMT)

Mtazamo huu unategemea hadithi kama ile inayosimuliwa na Umm Atiyyah, ambaye alisema kwamba wanawake waliokuwa kwenye hedhi waliambiwa wakae mbali na mahali pa kusalia/swalia wakati wa sala za Eid (imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim)

Surah Al-Baqarah (2:222), "Wanakuuliza habari ya hedhi. Sema: Huu ni unajisi. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka watwahare.( Tusilaumu sana yawezekana mlinzi wa kike alikuwa kwenye Surah Al-Baqarah 2:222 ).

Pia soma: Mlinzi wa kiume wa Rais kuvaa juba (vazi la kike) na kuketi msikitini sehemu ya wanawake ni sawa?
Kama ni jambo la kawaida mbona Shura ya maimam inataka maelezo??
 
Maelezo mengi na ya HOVYO. Ulinzi wa hivyo ni wa kishamba , INTELLIGENCE yetu ifike mahal ifanye kazi scientifically na sio traditionally kama hivyo. Why ulinzi wa Africa kwa PSU umefocus kwenye nguvu na physical attack . Tuna mambo ya ajabu ajabu snaa. Mimi naaamini kwa Africa hasa Tanzania, mtu akiwa seriously anataka kufanya tukio ni rahis na akafanikiwa.wewe una focus na gun na mabavu adui anakuja na pen ambayo ndani yake can emit strong poison. All those ambao hawajapata antidote itawaathiri from a distance of 100M, do we have technology to detect vitu kama hivyo, ?

Ulinzi wa hivyo ni kishamba na tukubali we need to learn tupo nyuma sana. Walinzi wa Rais wanapiga hela tu but nothing special , mimi huwa siku zote nawaona Kama wapambe but not really security, may be we are not that potential ndio maana no one bother with us but kama tungekuwa potential, wabaya hawashindw kufanya watakalo

We are too traditional than scientifical
Mbwelbwe nyingi, but we are not that serious . Mmeona ndege ya Iran ilivyo chepushwa kutoka kwenye msafara wa helicopters, and specifically imekuwa pointed iliyombeba Rais na ikawekwa kando. Mengine yakabaki history . Hakuna gun hakuna mabavu. Kwa sasa hayupo tena kazi imeisha : tangu mwanzo aliambiwa, ulishawahi kupiga kambi ya USA wakati yule mkuu wa majeshi wake alipouliwa na dogo tu wa 16 years ambae amekuwa trained kuchezea drones . Raisi akaambiwa , this time ukijibu kwa namna yoyote, we will get busy with you .Israel ni USA and we have strong military logistics. Jama akaleta ubishi wa kishia…. Mengine yamebaki hadith.

Dunia ya Sasa Vita ipo kwenye science na machine programming learning
Sisi bado tunapasua Tofaul, kuvaa suti na miwani nyeusi.

Mpaka Rais anaenda mahali, kwa wenzetu , scientifically hilo eneo ni proven kuwa ni salama , na hakuhitaji msururu wa watu named as walinzi wanaofikia hatua ya kuvaa hijabu, that is really awkward Hata miaka ya 70s sidhan walikuwa wanafanya hivyo
. Sasa mbona una hasira zisizo na maana kiongozi...

. Sijakataa unachosema, niambie hizo technology ulizozungumzia hapo juu kwa hapa Africa ni taifa gani linatumia 🤔🤔.


. Hizo mbinu/mbino za sijui pen umejuaje kuwa hapa TANZANIA hazipo???
 
Tembea. Ni vile seems you are not well informed . Hakuna huo ulinzi unaosema

Labda unazungumzia fujo za kisiasa but fujo za Maisha zipo mno
Watu wanakufa pasipokuwa na tija na taarifq huzipati
. Fujo za Maisha hizo ni kawaida kuuana, mfano huwezi kuzuia mtu kujinyonga au kuchomwa kisu.
 
Kama ni jambo la kawaida mbona Shura ya maimam inataka maelezo??
. Unaweza kuwa mwanadini lakini usielewe mipaka ya dini, mila pamoja na jamii inavyotakiwa kuendeshwa.

. Ningeona hao akina ashura/shura wanaakili zaidi kama wangeambatanisha na vifungu vya maandiko ya Quran, ( lakini umejionea mwenyewe kilicho andikwa)
 
Back
Top Bottom