Rais Samia kuipa Taifa Stars Tsh. Bilioni 1 ikishinda ubingwa wa CHAN 2024

Rais Samia kuipa Taifa Stars Tsh. Bilioni 1 ikishinda ubingwa wa CHAN 2024

Mama kaahidi sababu anajua kichwa cha mwendawazimu hakifiki popote
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa shilingi bilioni 1 kwa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania (Taifa Stars) endapo itafanikiwa kutwaa ubingwa wa CHAN 2024 na kubeba kombe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi, amesema hayo leo July 24,2025 wakati akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ufunguzi wa fainali za CHAN 2024 Tanzania vs Burkina Faso utakaochezwa Auguts 2, 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Katika kuchagiza hamasa kwa Timu yetu ya Tanzania, Rais Samia ametoa ahadi ya donge nono la fedha Tsh. bilioni, sio milioni ni bilioni yaani mabii, bilioni 1 kwa Vijana wetu wa Taifa Stars, iwapo watafanikiwa kutwa ubingwa wa mashindano haya ya CHAN 2024, Mcheza kwao hutunzwa na yeye ameamua kuwatunza"

View attachment 3416997
Chanzo: Millard Ayo
Kiswahili sanifu ni mcheza kwao hutuzwa✓ na siyo hutunzwa× !
Mzizi wa neno hapo ni tuzo ✓ na siyo tunzo×.
Maana yake mcheza kwao hupewa tuzo na ndiyo maana ya kutuzwa!
Sasa vilaza wengi utasikia mcheza kwao hutunzwa!!
Baraza la Kiswahili sijui lilifia wapi?!
 
Lengo ni nini? Timu ya Taifa haitakiwi kuhadiwa mapesa bali wanatakiwa kujituma ,kama wanategemea mshiko ili wafanye vizuri sio wazalendo na wafungwe tu
Tupe mfano wa timu ambayo inafanya vizuri bila ahadi ya mshiko
 
Hizi fedha huyu mama huwa anazitoa wapi ?
Ni za kwetu mimi, wewe, huyo, yule na hawa, na waleeeee

Bahati nzuri hatunaga mishipa ya hasira kabisa kwenye miili yetu, hata akijichotea kununua mabasi, pikipiki na baiskeli za kijani wala hatuna shida. Kwanza hizo hela huwa tunamgawia Bure na kuziita za kwake.
 
Zako we mlipa Kodi ? Ukiachana na kodi za kwenye vocha
 
Back
Top Bottom