Nianze hapo. Kumeibuka taswira halisi na Kali baada ya kugusia Katiba Mpya na mikutano ya siasa. Ni kama imeficha mema yote uliyofanya Kwa Siku 100 ulizokaa madarakani.
Sifa zote ulizopata zimefichwa. Mama yetu mpendwa hio ndio taswira ya ukubwa wa tatizo lililopo.
Watakuja makada na washauri wako kupitia taasisi zao wajipendekeze na kukudanganya usione huo ukweli.
Wanasiasa ni wahanga wakubwa Wa awamu ya 5. Na hadi sasa hawajapata tiba sahihi na matumaini.
Hawajasikia kuhusu watu walioteswa, kuuwawa na kupotezwa. Hawa wengi ni wanasiasa. Hawajasikia mwelekeo Wa chaguzi zilizovurugwa Kwa makusudi. Hawajasikia kuhusu Tume ya uchaguzi na usimamizi Wa Wakurugenzi. Hawajasikia Namna Polisi na vyombo vyengine vikitajwa na kuwajibishwa Kwa kutumika kisiasa. Mambo yako wazi mama. Mifumo na sheria za kusimamia haki hazijaguswa kimya.
Katika hali hio, tumaini ni Katiba Mpya na kufuatwa sheria ya vyama vya siasa. Leo unapokuja na kauli zile unatonesha vidonda na kuyakwaruza makovu Kwa viwembe.
Nadhani ujumbe baada ya kauli ile umefika. Nia yako njema kwa Taifa hili inatazwa na hayo mawili.
Jitahidi kuwa makini na washauri wako. Taifa ni kubwa kuliko CCM. Wanasiasa Kwa umoja wenu ndio hutoa taswira ya nchi. Malalamiko yao hufika haraka kote duniani na nchi kuwekwa rehani.
Hili kundi lina wafuasi wengi na ukweli ni kwamba liliteseka mno.
Jitahidi kuvumilia kama ulivyo, na jitahidi ku-balance mambo.
Nchi hii ni ya wote. Kumbuka ule msamiati kwamba cheo ni dhamana na daima tenda mema uwende zako.
Nawasilisha.
Kishada