Chozizwa2020
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 912
- 853
Mkuu umenena vyema, lazima tuambiane ukweli! Siasa ni KILA KITU. Ndio maana Hayati Mwalimu Nyerere alipata kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu 4: WATU, ARDHI, VIONGOZI BORA na SIASA SAFI.Kimsingi ukiumiza wanasiasa umeumiza watanzania. Hakuna mtanzanua haguswi na siasa ndio maana kila mahali tulifurahi Samia alivyoanza siasa nzuri.
Hapa ukichambua utaona kuwa Watu wapo(Watanzania)Ardhi ipo tena kubwa ya nchi ya Tanzania; Viongozi Bora, hawa wanatokana na Watanzania wenye elimu, maarifa na ujasili na kuwekwa uongozini na Watanzania wenzao na mwisho Siasa Safi. Siasa Safi huletwa na Viongozi Bora, wenye elimu, maarifa, hekima na ujasili, ambao sio wabinafsi, sio wala rushwa na wanafiki.
Siasa Safi huleta maendeleo katika Nchi, bila Siasa Safi Nchi haiwezi kupata maendeleo yanayotarajiwa. Kwa mantiki hiyo SIASA ndio DIRA au mpangilio wa shughuli za mwanadamu/mwananchi katika kufikia malengo yake ya maendeleo.
Nchi ikiwa na Siasa Safi itaendelea (itokanayo na viongozi bora) na ikiwa na Siasa mbovu haitaendelea (itokanayo na bora viongozi) Hivyo basi SIASA NDIO MPANGO MZIMA KATIKA MAISHA YA BINAADAMU YA KILA SIKU