Rais Samia, kujua ukubwa wa tatizo kutasaidia kuliponya; kundi la wanasiasa liliumizwa sana

Rais Samia, kujua ukubwa wa tatizo kutasaidia kuliponya; kundi la wanasiasa liliumizwa sana

Kimsingi ukiumiza wanasiasa umeumiza watanzania. Hakuna mtanzanua haguswi na siasa ndio maana kila mahali tulifurahi Samia alivyoanza siasa nzuri.
Mkuu umenena vyema, lazima tuambiane ukweli! Siasa ni KILA KITU. Ndio maana Hayati Mwalimu Nyerere alipata kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu 4: WATU, ARDHI, VIONGOZI BORA na SIASA SAFI.

Hapa ukichambua utaona kuwa Watu wapo(Watanzania)Ardhi ipo tena kubwa ya nchi ya Tanzania; Viongozi Bora, hawa wanatokana na Watanzania wenye elimu, maarifa na ujasili na kuwekwa uongozini na Watanzania wenzao na mwisho Siasa Safi. Siasa Safi huletwa na Viongozi Bora, wenye elimu, maarifa, hekima na ujasili, ambao sio wabinafsi, sio wala rushwa na wanafiki.

Siasa Safi huleta maendeleo katika Nchi, bila Siasa Safi Nchi haiwezi kupata maendeleo yanayotarajiwa. Kwa mantiki hiyo SIASA ndio DIRA au mpangilio wa shughuli za mwanadamu/mwananchi katika kufikia malengo yake ya maendeleo.

Nchi ikiwa na Siasa Safi itaendelea (itokanayo na viongozi bora) na ikiwa na Siasa mbovu haitaendelea (itokanayo na bora viongozi) Hivyo basi SIASA NDIO MPANGO MZIMA KATIKA MAISHA YA BINAADAMU YA KILA SIKU
 
Nasikitika kwamba aw amu ya 5 ya utawala Wetu ulitengeneza tatizo kubwa sana. Licha ya Kabla ya napo Ku we po matatizo Lkn wat u walivumiliana. Leo mama atalazimika kuvumilia Tu. Ili watu watoe dukuduku ndipo turudi kwenye mstari.

Hatujachelewa
 
Prof Asad kasema katiba ni muhimu hata kwa Rais mwenyewe wala haitampungukia kitu zaidi itampaisha kisiasa; nakubaliana naye.Tatizo ni kwa wabunge waliobebwa 2020 wanadhani huo ndio utakuwa mwisho wao
 
Prof Asad kasema katiba ni mhimu hata kwa Rais mwenyewe wala haitampungukia kitu zaidi itampaisha kisiasa; nakubaliana naye.Tatizo ni kwa wabunge waliobebwa 2020 wanadhani huo ndio utakuwa mwisho wao
Mpaka sasa watawala hawajajifunza somo LA uvumilivu LA watanzania.

Wanatafakari zaidi maslahi binafsi na kutumia misuli ya dola ilimradi ni tiifu kwao.
Kesho yetu hatuijui tutumie nafasi kuweka mazuri.

Kundi LA wanasiasa liponywe Kwa njia sahihi sio kuumizana
 
Back
Top Bottom