Rais Samia kukopa(tena) 1billion USD from IMF

Kama ambavyo nimeeleza awali, sina haja ya kubishana na wewe. Mimi niliishia std 2 wewe ni mchumi mbobevu.
 
Yaani basi tu hii nchi Kama vipi mikoa ijitenge iwe nchi. Wapo wengine watabidi wajiuze kabisa kwa wenye mikoa mingine yenye nguvu na chakula na madini ya kufa mtu.
Yaani tungewabana kabisa kwenye madini na gesi miktaba ingekaa kimaslahi na sio kutajirisha Koo fulani nadhani tungeenda mbali Sana.
 
Unawajua miongoni mwa walaji au una hamka.tuu?

Kwenye miradi ya P4R inayotolewa na wafadhili kwenye maji na elimu wameamua kuongeza ufadhili wao baada ya kuona matokeo mazuri ya usimamizi wa Fedha.
 
Kwa hiyo wewe unaona ni pesa nyingi sana hiyo sio? Yaani Til.2 ndio imekuchanganya? Maskini wa akili na mali 😄😄

Aisee Machadomo kichwani hamna kitu khaa,hivi unajua bajeti yetu ni dola bil.ngapi?
Kama 2 trilion ni kidogo Kwanini mnataka kukopa fedha kidogo?
 
Unawajua miongoni mwa walaji au una hamka.tuu?

Kwenye miradi ya P4R inayotolewa na wafadhili kwenye maji na elimu wameamua kuongeza ufadhili wao baada ya kuona matokeo mazuri ya usimamizi wa Fedha.
Huko MSD ambako waziri mkuu anadai 215 milion zimeliwa na watumishi watatu,huoni huo ni ushahidi kua pesa zinaliwa hovyo,na wahusika hawachukuliwi hatua stahiki?
Unafikiri kipindi cha Magu ingeishia kusema tu hivyo?
Mama naye anasema wale kulingana na urefu wa kamba zao,huoni huo ni uhalalishaji wa utafunaji pesa?
Utakua ginger kama unahitaji ushahidi wowote.
 
Bi mikopo yuko kazini. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani walivyokula wameachwa?
 
Mama tafuta pesa tunakutia moyo,vijana hawawezi ajiriwa bila pesa
 
Zanzibar wanatabasamu kwa mgao ujao japo kwenye kuulipa hawatahusika maana chao ni chao ila chetu chao 😁😁
 
Nikushukuru sana mkuu 'Titicom' kwa mchango wako huu mzuri.

Hizi "austerity measures" hawa jamaa wanapenda sana kuzitumia mara kwa mara. Juzi wamejaribu kuwalazimisha Kenya wasiweke ruzuku kwenye mafuta, Kenya wakawagomea, na bado wanaendelea kutoa pesa.

Kwa hiyo, hizi 'austerity measures' zinajadilika; mradi tu tuwe na viongozi wajanja,kama huyu tuliye naye, badala ya kutumia lugha kali kukataa matakwa yao, anawalainisha kwa lugha nyororo, huku tukiendelea kugoma kulipa deni lao.

Jambo muhimu ambalo ninalikazia hapa, ni hiyo mikopo tunayoichukua kutoka kwao iwe imefanya kazi iliyopangiwa na kuikamilisha vizuri; halafu, hatukatai kabisa kuwa tuna deni nao, ila tunalipa kufuatana na uwezo wetu.

Tatizo ninaloliona kwetu, ni kuchukua mikopo, kama huu wa bilioni ya kulipa ruzuku ya mafuta. Mikopo kama hii ni ya kipuuzi kabisa.

Sijawahi kusikia wakichukua mkopo kwa ruzuku ya mbolea ili wakulima wetu wafanikishe kilimo! Hata wakichukua mkopo kama huo ni sehemu ndogo tu ya pesa inayotumika kununulia mbolea, na kiasi kikubwa hakijulikani kinapokwenda. Haya ndiyo matatizo yetu.
 
Kwenye miaka ya 1950, Korea ya Kusini na Tanganyika zilikuwa sawa kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…