Rais Samia kumpokea Rais wa Guinne Bissau Ikulu hapo kesho

Rais Samia kumpokea Rais wa Guinne Bissau Ikulu hapo kesho

Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam
Naona ikulu ya Dodoma mmeamua kuisusa.
Gharama zote za kuijenga na zile kelele za kuhamia Dom zimeshasahaulika.
Ccm zimwi..!
 
Naona ikulu ya Dodoma mmeamua kuisusa.
Gharama zote za kuijenga na zile kelele za kuhamia Dom zimeshasahaulika.
Ccm zimwi..!
Ikulu zote zinatumika bila shida yoyote ile maana zote ni zetu na hakuna ambayo tumepanga.
 
Mwanaharakati Amilcar Cabral, pamoja na 'mistari' yake mashuhuri ya kuwasilisha ujumbe kwa umma :

Yusra Buwayhid
25.07.201825 Julai 2018
Akiibuka kutoka kundi la wapigania uhuru wa Afrika, Amilcar Cabral ameiongoza Guinee Bissau na Cape Verde kuelekea uhuru kutoka watawala wa kikoloni wa Ureno. Lakini aliuliwa kabla ya kulifikia lengo lake.

SIASA

Kutana na Cabral aliyepigania uhuru kutoka ukoloni wa Ureno​

1719031975405.png


01:26

SIASA
Yusra Buwayhid
25.07.201825 Julai 2018
Akiibuka kutoka kundi la wapigania uhuru wa Afrika, Amilcar Cabral ameiongoza Guinee Bissau na Cape Verde kuelekea uhuru kutoka watawala wa kikoloni wa Ureno. Lakini aliuliwa kabla ya kulifikia lengo lake.


MATANGAZO

Amilcar Cabral ameisihi muda gani?
Amezaliwa mwaka 1924 mjini Bafatá , Guine Bissau. Wazee wake walitokea Cape verde. Amekulia Sao Vicente
,Cape verde na kusomea fani ya kilimo mjini Lisbone. Alirejea baadae Guinea Bissau. Aliuliwa january 20 mwaka 1973 mjini Conakry nchini Guinea.
Kwanini Amilcar Cabral alikuwa maarufu?
Akiwa muasisi mwenza wa chama cha waafrika wanaopigania uhuru wa Guine na Cape Verde (PAIGC), mwaka 1956, Amilcar Cabral alichaguliwa akuwa katibu mkuu na kuziunganisha nchi hizo mbili katika mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ureno. Chama cha PAIGC kikaiongoza Guine Bissau hadi uhuru mwaka 1973.Cabral alikuwa mpigania haki za Afrika, alikuwa pia mtaalamu wa kilimo na mtunga mashairi..Hakuwa akikubali kuigiza mitindo ya kigeni ya mapambano ambayo kwa maoni yake hayambatani na mitindo ya amani ya Guine Bissau.

Amilcar Cabral kavutiwa na nani na amewavutia akina nani?

Amilcar Cabral ameyavutia makundi menegine ya ukombozi katika nchi zinazozungumza kireno barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla. Amechangia katika kuundwa kituo cha-Centro de Estudos Africanos, jumuia ya wanafunzi wa kiafrika wanaozungumza kireno na alikuwa na maingiliano na viongozi mashuhuri wapigania uhuru wa nchi za Afrika zinazozungumza kireno mfano wa Agostino Neto, Mário Pinto de Andrade, Marceelino dos Santos.

'Mistari' ya hoja mashuhuri za Amilcar Cabral:

"Waafrika wanatambua kwamba nyoka hata akijibadilisha ngozi, lakini anabakia kuwa nyoka."

"Hatujawahi hata mara moja kuwachanganya chungu kimoja "ukoloni wa Ureno na wananchi wa ureno". Mapambano yetu ni dhidi ya ukoloni wa Ureno."

"Atakaetaka kuniumiza atakuwa pamoja nasi, hakuna yeyote atakaekidhuru chama cha PAIGC isipokuwa sisi wenyewe."

Nani kamuuwa Amilcar Cabral?

Amilcar Cabral ameuliwa mjini Conakry na mwanachama wa chama chake mwenyewe anaesemekana kapokea amri kutoka Ureno. Lakini maafungamanio hayo yamezusha eti eti nyingi kuhusu nani hasa anabeba jukumu la kifo cha Cabral. Kuna wanaposema aliyemuuwa Amilcar Cabral anajulikana lakini aliyeamuru auliwe hajulikani.


Makala hii kwa hisani kubwa ya DW pamoja na :
Carla Fernandes and Gwendolin Hilse wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.

Mwandishi:Fernandes,Carla/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Yusuf Saumu
 
"Maneno matupu ya kumkera mkoloni bila ushiriki katika harakati za mapambano kwa vitendo hayaweze kutokomeza Ukoloni mkongwe na ubeberu" - Amilcar Cabral

"We are not going to eliminate imperialism by shouting insults at it." ~ Amilcar Cabral
1719032846613.png

Picha : Amilcar Cabral akiongoza mapambano Guine Bissau dhidi ya ukoloni mkongwe wa Kireno.
Image and article courtesy of Mshana Jr : Africa history made (Marejeo)
 
Ndugu zangu watanzania,

Naomba nisiwachoshe wala kuwapotezea muda wenu.someni wenyewe hapa chini.

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam ambae atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru.
Ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru.

Wakati wa ziara hiyo, Marais hao wawili wanatarajia kuongoza mazungumzo rasmi ya kiserikali kati ya Tanzania na Guinea-Bissau na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano (General Framework Agreement) ambao utaongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Mbali ya mazungumzo na Rais Samia, Rais Embaló atatembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Makao Makuu ya Sekretarieti ya Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) yaliyopo hapa nchini, ambapo yeye ni Mwenyekiti wa ALMA.

View attachment 3022535

View attachment 3022540
Umaro Sissoco Embaló, Rais wa Guinea Bissau
Masikini na masilini mnajadili nini ? Kuiba kura mbaki madarakani milele ? Non sense....tunataka wawekezaji viwanda vitoe ajira.....wananchi wengi
 
Dora the explorer alivyo mkarimu baada ya kumpokea anaweza kujitolea kumsindikiza pia huyo mgeni mpaka nchi yake na akafikia huko akajialika kwa ziara ya 3 huko huko.
 
Back
Top Bottom