Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Raisi Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri ambalo ni lilelile alolirithi kutoka kwa mtangulizi wake hayati Magufuli.
Ni mabadiliko ambayo yanaonyesha kwamba anataka watu wataomsikiliza na walo tayari kufuata akitakacho na si kujitia ujuaji.
Hivyo raisi kaamua kumuacha Dotto Biteko aendelee kuiongoza wizara ya Madini licha ya kelele na kampeni nyingi za kutaka waziri huyo aondolewe.
Dotto Biteko ameonyesha kiwango cha juu cha uchapakazi katika wizara hiyo ambayo ni moja ya wizara nyeti.
Hivyo kwa hapo nampa kongole raisi Samia na naomba uendelee na Dotto Biteko hadi utakapomaliza muda wako.
Profesa Mkenda aliwahi kutofautiana kauli na raisi Samia lakini ikaonekana ile ilikuwa ni mapungufu tu katika kuboresha hoja na wakayamaliza. Hii pia yaonyesha ukomavu na uelewa mpana alo nao raisi Samia na kwamba yupo tayari kuketi na kutafakari juu ya mawaziri ambao anadhani wanaweza kumsadia.
Profesa Mkenda anafaa kuongoza wizara ya elimu, Sayansi na teknolojia kwani wizara hiyo inahitaji mtu ambae anaweza kufanya marekebisho khasa kwenye suala la mitaala ya ufundishaji.
Pia Waziri Mkenda ataangalia namna ya kuboresha masomo ya sayansi na pia kupata vijana mahiri katika masomo ya sayansi ambao watasukuma mbele nchi yetu katika masuala ya sayansi, tehama na teknolojia.
Hussein Bashe kijana mwenzangu ni kijana makini sana na nafikiri alibinywa kiaina katika azma yale ya kutaka kukibadili kilimo cha mtanzania. Huu ni wakati wa Hussein Bashe kuhakikisha anasimamia mapinduzi ya kilimo kiwe cha kisasa na chenye kumsaidia mkulima wa kitanzania.
Waziri Bashe pia aangalie suala la pembejeo za kilimo na uagizaji mbolea kutoka nje. Kama tuna kiwanda cha mbolea hapahapa nchini ni budi kuongeza tozo kwa mbolea inayotoka nje ili mbolea inayozalishwa hapa nchini ipate soko na iwe ni kitendo cha kujivunia kuzalisha mbolea yetu wenyewe.
Siku hizi kuna masuala la "food Security" ambapo hiki ni kipimo cha uwepo wa chakula na uwezo wa wananchi kukipata chakula hicho bila shida, kwa kifupi uwezo wa nchi kujilisha.
Dada Ummy Mwalimu umerudishwa wizara ya Afya na hii ni muhimu kuzingatia. Wizara kwa sasa ina changamoto ya ugonjwa wa COVID-19. Ni wakati sasa wa kufikiria kuanzisha taasisi ya usalama wa Afya yaani Health Security Agency. Taasisi hii itapanga na kusimamia magonjwa ya kuambukiza yanayotoka nje ya Tanzania, na itafanya kazi na bodi ya kisayansi (sidhani kama nayo hii ipo) kubaini aina mpya za virusi vya magonjwa ya milipuko.
Pia itafuatilia kwa makini wasafiri wa kimataifa na kuchungua zile pasi wanozijaza kabla ya kusafiri kubaini wamepita wapi na wapi,usimamizi wa vifaa na chanjo za magonjwa kama COVID-19 na kufanya test and trace kwa wagonjwa.
Haya yote yawezekana kwa kuzingatia kuwa fedha zipo na tulipewa zile za COVID-29 au pendemic, hata hivyo hongera sana kwa kurudishwa wizara ya Afya.
Mwisho ni uteuzi wa mdogo wangu Mchengerwa kuwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kwa kuwa nchi hii hadi sasa inaeleweka kuwa ni ngumu kuiongoza basi mheshimiwa Mchengerwa ni budi utafakari juu ya kurudisha kombe la taifa ili kuweza kuwakutanisha watanzania na kuwawezesha kusahau yalopita na kuganga yajayo.
Kombe la taifa litafaa lifanyikie Dodoma ili kuweza kusukuma fedha kwenda kule na kisha kuufurahisha mji huo makazi rasmi ya serikali yetu ya JMT.
Kombe la taifa lilaleta mshikamano baina ya watanzania ambao hadi sasa wamegawanyika kutokana na masuala ya kisiasa yanoendelea.
Kombe la taifa linahitaji wadhamini ambao si kazi ngumu kuwapata na endapo watapatikana wadhamini basi pia utawaomba wadhamini michezo mingine kama UMISETA, UMISHUMTA na baadae urudishe michezo ya ushindani khasa kama Netball, Volleyball ili angalau kama taifa tuweze kucheza kwenye ngazi ya kimataifa.
Nchi hii ni ngumu yenye historia ya kipekee kabisa katika bara la Afrika na hadi leo tunaheshimiwa sana kwa aina ya uendeshaji wa siasa zetu, lafudhi ya lugha yetu tukufu la kiswahili na hata vyakula ambavyo huwachanganya sana wageni.
Kila la kheri Raisi Samia na baraza lako jipya la mawaziri bila kumsahau kamanda na mzee wangu kapteni George Huruma Mkuchika bado wewe ni mtu makini sana na sehemu ya macho ya nchi hii.