Sasa kuna tatizo. Kutokana na tatizo la mabadiliko ya mazingira (climate change), mataifa makubwa duniani yameweka mkakati wa kuacha kutumia mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. Norway kwa mfano, wanasema kufikia 2050 wataacha kabisa shughuli za kuchimba mafuta. Uingereza wanasema watapiga marufuku magari ya kutumia diesel kufikia 2025 nadhani. Japan, Germany na hata China, wote wanasema ndani ya miaka 15 ijayo wanataka kutoka kwenye kutumia mafuta kwenye magari na kuingia kwenye magari ya umeme (from internal combustion engines to electric vehicles)
Sasa hii inamaanisha nini kwa nchi kama Tanzania ambazo hadi sasa zimekalia tu uchumi wa mafuta bila kuuendeleza? Ina maana ndani ya miaka 20 ijayo, mafuta yatakuwa si mali kitu. Hata ukigundua una mafuta mengi kama bahari ya Hindi, hayatakusaidia tena kwa kuwa dunia imeanza kuondoka toka tekinolojia ya mafuta kwenda teknolojia ya umeme!
Hivyo basi, kama kweli tunataka kufaidika na rasilimali ya mafuta tuliyonayo, ni lazima iendelezwe ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo. La sivyo haya mafuta yatakuwa na rasilimali isiyohitajika tena duniani, na ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo tutaanza kushuhudia kuporomoka kwa bei ya mafuta kadiri magari ya umeme yanavyoingia sokoni. Leo hii hata Lamborghini wamesema wataacha kutengeneza gari za mafuta!