Rais Samia: Kuna makubaliano TANESCO na Shirika la umeme la Rwanda (REG) kuanza kuuziana umeme

Rais Samia: Kuna makubaliano TANESCO na Shirika la umeme la Rwanda (REG) kuanza kuuziana umeme

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame leo Mei 3, 2026.

Rais Samia amezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda, ikiwemo Mradi wa Umeme wa Rusumo unaohusisha Tanzania, Rwanda, na Burundi, Mradi huo unatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati 80 za umeme.

Alieleza kuwa tayari mradi huo umeanza kufanya kazi, na sasa wamekubaliana kuuzindua rasmi ambapo pia Mashirika ya umeme ya Tanzania (TANESCO) na Rwanda (REG) yameingia makubaliano ya kuanza kuuziana umeme ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.


 
Back
Top Bottom