Rais Samia: Kuna mambo hayakuwa yakifanyika, lakini sasa hivi yanataka kuanza. Sitokubali!

Rais Samia: Kuna mambo hayakuwa yakifanyika, lakini sasa hivi yanataka kuanza. Sitokubali!

Komaa mama, hayo mambo unayosema yanataka kuanza yameshaanza, mpaka yakufikie kwa kiwango unachotaka basi ujue huku site ujenzi umesimama kabisa.
 
acha akina mkwere wamdanganye tuu, akileta ujinga tuna mweka ndani kama tulivyo wasweka akina abdujumbe
 
Yameanza kutokea baada ya kumuona hawezi kuwajambisha wakulungwa.

Anakiri wazi kuwa watendaji walio chini yake wanamdharau.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika miezi michache aliyokaa kwenye Serikali ya Awamu ya Sita, ameona mambo mengi ambayo huko nyuma hayakuwa yakifanyika lakini sasa hivi yanataka kuanza, akisisitiza hatokubali

Amesema hayo baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Awamu ya Tatu, kipande cha Makutupora - Tabora

Amesisitiza ubora wa vifaa vinavyonunuliwa na Reli inayojengwa kuendana na thamani ya Fedha. Vilevile ameagiza Shirika la Reli (TRC), Wizara ya Ujenzi na wengine wanaohusika kusimamia Ujenzi huo
Mkuu mjenzi wa kipande cha Makutopora - Tabora bado ni Mturuki?
 
kwanini majaliwa asiwe moto ili kubalans jamani.

kama rais hana haiba ya ukali tusimlazimishe,basi ampe jeuri waziri mkuu ili amsaidie kudili na waharibifu..

Mimi nahisi tatzo ni utashi wake..naamini majaliwa akipewa rungu atawapukutisha mchwa wanaohujumu kazi yake..

Huku kupoapoa kwa majaliwa na wenzake kunaweza kuwa na sababu..

Haiwezekani Rais, makamu, waziri mkuu wote wakawa toothless.

yaani mawaziri mwenye kujiamini na mwenye kauli ni mwigulu na ummy tu! Wengne baki ni majongoo.
Wakiamua kufurukuta wanaitwa sukuma gang!

Kuna kundi la Jk limemzunguka mama ndio maana unaona kina Majaliwa wamejikalia kimya! Kundi hili la JK kina Makamba na Nape wameshamlainisha mama kiasi kwamba kila anachoambiwa anaitkia tu.
.
Sasa kuna hatari nchi itaanza kuliwa kama mchwa

Kama umesoma uzi wa yule jamaa anaitwa Magamba matatu nadhani utakuwa umeelewa kinachoendelea!
 
Maza kaza kidogo politeness ikizidi utashindwa kuwadhibiti wasaidizi wako
 
Anaongea maneno matupu, vitendo sifuri
Hapo ni sawa na kumuahidi mwanao pipi kila siku ukiondoka nyumbani anakulilia, unamwambia nikirudi nakuletea pipi, jioni vile kasahau na wewe hukununua hivyo maisha yanaendelea kwa njia hiyo na mwisho wa siku kila mtu anazoea na hakuna jipya.
 
Back
Top Bottom