RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Rais aliamua kuwa sehemu ya watu wasiopenda kulipa kodi na ndiyo baadhi yao wanafadhili mitandao ya kijamii kwa kumsifia kuwa anaupiga mwingi.
Wakati sasa umefika anajionea yeye mwenyewe ameweka tozo kwa wananchi bado pesa za tozo hazijamsaidia kitu chochote hazijulikani zinaenda kwenye miradi gani, juzi amekiri mwenyewe kuwa serikali yake haina pesa na amesisitiza kuwa lazima tukope na tulipe hapo alikuwa akizungumzia ujenzi wa reli ya sgr kipande kuanzia tabora hadi kigoma
Kwa maneno yake yale baadhi ya taasisi za serikali kaeni tayari kucheleweshewa mishahara maana kwa sasa mambo aliyonayo Rais ni mengi hasa ya kutekeleza miradi ya maendeleo, wakati mwingine ndiyo maana mama anatoka kidogo nchini yapo mambo mengi anapokuwa nchini anashindwa ashike lipi na aache lipi ndiyo maana anaamua kwenda kula upepo kule kwa wenzetu wanaotukopesha.