Rais Samia kunusuru zao la korosho

Rais Samia kunusuru zao la korosho

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Desemba 1, 2022 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishiriki maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani baada ya maadhimisho hayo alisimama na kusalimiana na Wananchi wa Mnazi mmoja mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Mtwara.

Dkt. Samia Suluhu alitoa nafasi kwa mbunge wa Mtwara kutoa salamu, moja ya jambo lililozungumziwa na Mbunge wa Mtwara ni kushuka kwa Bei ya korosho, Rais Dkt. Samia alimuita Waziri wa Kilimo kulitolea majibu nae Mhe. Hussein Bashe akaelezea mpango wa Serikali kuwanusuru wakulima wa Korosho pamoja na zao la Korosho ambalo ndio tegemezi la Uchumi wa Kusini.

Waziri Bashe alikiri kushuka kwa bei ya Korosho nchini na kusema si tu Tanzania pekee isipokua bei ya Korosho imeshuka katika soko la dunia. Mipango ya serikali ya awamu ya sita ni 👇
  • Uwazi kwenye uuzaji wa Korosho kwenye minada​
  • Kuuza Korosho ambazo tayari zimeshabanguliwa "Bei ya Korosho imeshuka duniani, mheshimiwa Rais ametupa maelekezo tuanze kubangua korosho na sio kuuza korosho ghafi, tumeanza na tumeuza tani 7 Marekani" -Hussein Bashe​
  • Kuvirejesha viwanda zaidi ya 10 vya kubangua korosho vilivyofungwa​
  • Ujenzi wa kiwanda kipya cha Korosho​
  • Kugawa mashine ndogo ndogo za ubanguaji Korosho kwa wakulima​
  • Kuwawezesha wakulima walime mazao mengine kama Ufuta na Soya badala ya kutegemea korosho pekee.​

1670245532898.png
 
Rais Samia Suluhu ameweka nguvu kubwa katika sekta ya kilimo.
 
Back
Top Bottom