Rais Samia kupokea ndege mpya ya ATCL Julai 30, 2021

Rais Samia kupokea ndege mpya ya ATCL Julai 30, 2021

Kwa hiyo mkusanyiko wa kesho ni muhimu japo watu wametahadharishwa kuepuka mikusanyiko isiyokua ya lazima
Daaaaaah sisi tunalazimishwa kwenda kwenye mkesha wa mwenge. SIJWAELEWA kuwa kirusi kinachagua mikisanyiko au?
 
Hivi hawa watu hua wanatuonaje?
CAG anaongea hadi koo linakauka anagonga glass ya maji ya baridi mbele ya kamera akisisitiza shirika letu la ndege ni hasara mwanzo mwisho...tukiwa bado tunaugulia maumivu ya tozo, unapigwa kanzu na mapokezi ya dege jingine.
Ndege zilishalipiwa na magufuli na alitamka mwenyewe hivyo zilikua zinasubiri zihe nchini
 
Ndege zilishalipiwa na magufuli na alitamka mwenyewe hivyo zilikua zinasubiri zihe nchini

Sina tatizo na hilo na nnalifaham kwamba ndege zilishalipiwa. Ikumbukwe mara baada ya JPM kuhitimisha safari yake hapa duniani, kuliibuka makundi na tuhuma kadhaa akiwepo CAG kutoa taarifa ya ubadhilifu kwenye ATCL...tukaaminishwa manunuzi ya ndege yalikua maamuzi yasiyo na uzito.

Kwa watu wanaomaanisha wanachokisema na kusema wanachomaanisha, ndege kuja itakuja tu hata bila kupokelewa kwa mbwembwe.

Nnachokiona waimba mapambio ni kama badi wanatafuta channel gani inakamata mawimbi ya Mama waende nae sambamba kwenye vibwagizo vya mapambio.
 
Back
Top Bottom