Rais Samia kuruhusu watu wajadili mkataba wa bandari tayari ni legacy

Wewe ni taahira
 
Hata kuuza bandari kwenyewe ni legacy
 
Sasa kwanini wengine wanakamatwa
Sasa kwanini wengine wanatishiwa
Sasa kwanini wengine wanazushiwa mambo ya ajabu ajabu?
Ama karidhia kishingo upande?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekupata kwa sehemu, na uliyoyasema ni kweli.

1. Je, huu mkataba husingevuja wananchi wangejua yaliyomo?

2. Mara tu ya mkataba kuvuja, ikatolewa siku moja ya kusikiliza maoni ya watu wanaonaje huo mkataba, je ni wangapi walikuwa wameshauona na kuupiti ndipo waje watoe maoni?

3. Yawezekana anaacha watu walumbane, lakini maamuzi yaliyopitishwa ndiyo yatakayotekelezwa.
 
Idadi ya wapumbavu inaongezeka kwa kasi ya ajabu sana!

Ni vigumu kuamini watu mko wapumbavu kiasi hiki.

Maybe you’re not that stupid. Maybe you’re just trolling.

I hope [not with bated breath] that it’s the latter
Duh! Nyani Ngabu kumbe upo legendary!!!
 
Serikali haikuuleta mkataba ila wazalendo wa kweli waliuvujisha
 
Anaruhusu yeye kwa matakwa yake,au amelazimika kwakuwa sheria inamtaka kufanya hivyo kwa aina hiyo ya mkataba?
 
Legacy gani isiyokuwa na matokeo chanya?
 
Kwa aina hii ya mkataba ambao ni lazima uridhiwe na bunge hakuwa na namna, lazima tu angeupeleka bungeni na hapo ndipo mamba kama haya yangejulikana. Kama ungekuwa mi mkataba kama hiyo inayofuata inayoitwa host government agreements (HGA) tusingeujua maana hiyo si lazima ipite bungeni.
Na kwakweli hizo wanazoita HGA hutazijua maana hazitapelekwa bungeni.
Na hapo ndipo unapaswa kutofautisha mikataba mingine na huu na hapo ndipo tunapiga kelele maana mkataba kama huu unalazimisha kubadili sheria mbali mbali za nchi ili ziendane na mkataba - na huu ndiyo msingi wa marekebisho ya sheria mbali mbali uliopelekwa bungeni.
Kwa hiyo mkataba huu kupelekwa bungeni na kujadiliwa si hisani wa ridhaa ya rais bali ni matakwa ya kikatiba kwa mikataba ya aina hii.
 
Legacy gani isiyokuwa na matokeo chanya?
Na hii hoja ya Johari eti biashara ya siku hizi ni end to end yaani kampuni moja ifanye shughuli zote toka unakopatikana mzigo hadi unakoenda kwa mlaji, ni hoja mfu sana; ni kutengeneza monopoly ya kampuni moja.
Na hapo ametufunulia kwa nini kumbe DPW haihusiki na bandari za dar tu bali bandari zote hata za maziwa (lake ports) na pia na miundo mbinu yote ya kutoka bandari za bahari hadi kwa walaji (land locked countries. Ndiyo maana atapewa na bandari za nchi kavu nk.
Hakika hii ni kujifunga - shughuli yote hii ifanywe na kampuni kuwa moja tu DPW (au washirika/ wabia wake)? Yaani tunajifunga mikono na miguu na kuijenga kampuni moja badala ya kujenga biashra ya kiushindani? Hivi Johari uanelewa ubaya wa monopoly - utakuwa hufurukuti tena mbele yake atakachoamua huwezi kupinga maana utakuwa huna mbadala kila kitu ni yeye tu! Acheni hoja mfu zisizokuwa na mashiko
 
Legacy??? Basi ni ya kijinga Sana, Binadamu ana haki ya kutoa maoni na si Rais akubali au akatae
 
Idadi ya wapumbavu inaongezeka kwa kasi ya ajabu sana!

Ni vigumu kuamini watu mko wapumbavu kiasi hiki.

Maybe you’re not that stupid. Maybe you’re just trolling.

I hope [not with bated breath] that it’s the latter
Wewe NYANI kaa kimya.
 

Ameruhusu au mkataba ulivuja? Now ni damage control ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…