Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.
Saizi bidhaa za china zinajaa kwa gharama ya viwanda vya nani? Mna viwanda nyie au ni vya investors? Wao wataji tune kuendana na bit.

Kwani EPA ni kuruhusu bidhaa kutotozwa Kodi?

Lakini bidhaa za China na kwingineko angalau tunatoza kodi haziji na kuuzwa bila kodi!
 
wenzio huku west africa juice zao nyingi za kutoka Europa. Wenye viwanda kazi kwao hili washindane na imported goods. Je mazao yetu yana kiwango cha kushindana na wakulima wa mabeberu au ndo tutauza tu kwa wenzetu hapa Africa?
Bora kunywa juice kutoka ulaya IQ inatengamaa kuliko juisi ya mswahili mwenzako ambayo haina vigezo
 
Kwanza umekurupuka. Unaongea uvumi, pili unatakiwa kuweka mkataba hapa na sio kuongea kishabiki. Hatuwezi kuchangia uzushi na bila vielelezo. Kama ni mawazo yako binafsi sema kwamba unaongea bila kujua mkataba ukoje.
Lakini mbona umeshachangia..
 
Haki yake kwani Nani alimchagua
 
Nimejikuta nimemkumbuka Nazir Karamagi na mkataba wake aliosaini hotelini London awamu ya 4.

Ok sawa, ngoja niendelee kusoma kitabu cha Mwl Nyerere "Uongozi wetu na hatma ya Tanzania"
Hicho kitabu napata wapi?
 
utaratibu wa kusaini mkataba kwani umekaaje? maana huwa napata shida sana juu ya mikataba inayosainiwa na viongozi wa nchi hii, yaani ingependeza kwamza mikataba yote ipitie bungeni na kwa mwanasheria mkuu wa serikali, lakini cha kusikitisha hii nchi akija tu muwekezaji ataitwa waziri mwenye dhamana watakaa na kufanya mazungumzo yao, wakimaliza waziri anaanguka sain baadae tunaanza kupamba tu vichwa cha habari magazetini kwamba tumeshampata mwekezaji.....hii nchi ya hovyo sana
 
Kwa gharama ya Viwanda vyetu ? Vipi kuhusu ajira za watu wetu waliojiriwa kwenye hivi viwanda vyetu? Vipi kuhusu mapato ya kodi tunayoyapata sasa hivi kwa kutoza kodi imports ? Nani atafidia hiyo yote ?
kama viwanda vyetu vinatuuzia bei ghali vife tu, kama ni ajira tutafanya uchuuzi wa bidhaa za ulaya
 
Eti viwanda vyetu?
,Viwanda vya maji na juisi zenye kiwango Cha chini kabisa.
Viwanda ni vya Azam TU na anauza kokote.

Ukipita kariakoo bidhaa zote ni Mchina tupu na ubora hafifu. Mapikipiki yote Mchina tupu. Kila kitu kinatoka china bila mkataba wowote zaidi ya uhuni wa kujaza mpaka vifaa feki vya umeme na majiko ya gesi feki.

Bora ziingie bidhaa za ulaya nazo ili za china ziuzwe bei inayoendana na udhaifu wake. Hivi bajaji kweli inafaa kuuzwa mil. 9.? Pikipiki zilitakiwa ziuzwa mil. 1.5 zinauzwa mil.3. wakati ubora ni hafifu. Yote ni Kwa sababu soko la Asia limetawala Afrika. Mitumba Sasa ivi inatoka China tuu Kwa viwango hafifu bei kubwa.

Hakuna bidhaa inayoingizwa popote Duniani bila kulipiwa ushuru. Kinachafanyika ni kuruhusiwa Kwa masharti nafuu. Ni sawa na tunapozuia bidhaa kama sukari kuingia Toka Brazili. Sio kwamba hailipiwi Kodi Bali ni Kwa ajili ya kuharibu kulinda majizi na Mabeberu ya ndani yanayouza bidhaa ghali wakati Mali ghafi zipo na wanalipa wafanyakazi mishahara midogo . Hawa dawa yao ni kuwaletea ushindani TU mana hawana maana.
Mfano Sementi inauzwa ghali kuliko Ile iliyozalishwa Uarabuni na kutozwa Kodi Huko na kusafirishwa maili nyingi. Tatizo watanzania wanataka kuzalisha kidogo wauze Kwa bei kubwa wapate faida kubwa . Wezi wakubwa!!
Acha Magari used ya BMW Toka Ujerumani nayo yateke soko la japani ili Yale dhaifu yashuke bei.
Dunia ni Kijiji bidhaa inaweza kuzalishwa popote alimradi inampa binadamu unafuu wa maisha.
Kila kibidhaa ya Tanzania ni dhaifu mpaka Panadal huwezi Kulinganisha na Ile ya Kenya. Tatizo Nini wanatudharau sana wawekezaji Toka Asia.
Acha Mabeberu wa Ufaransa nao walete teknolojia yao. Tumechoka kufanywa kichwa Cha mwendawazimu. Soka tunakimbilia ulaya lakini bidhaa tunakimbilia midoli ya Chama na pipi na biscuit zilizojazwa chokuleti zimepangwa kwenye mitaro Toka China.
 
Bidhaa zitatoka ulaya Kama finished product, no need for electricity. Kwa hiyo viwanda vingi vitafungwa sababu bidhaa Toka nje hazilipi Kodi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…