Nimesoma na kusema ilkabidi nicheke tuu! Kusema kweli Rais wetu si mwenye tabia ya kusoma vitu hata kidogo! Sitashangaa yeye akisaini kwakuwa kaambiwa! Rais wetu yeye huwa akikutana na mkataba ni kusaini tuu wala sina hakika kama anao muda wa kusoma hata kidogo.
Rais Samia ana udhaifu wa kutopenda kufatilia kujipa muda wa kujitafakari na kupitia mambo yeye huwa ni mtu wa kuanguka tuu sahihi hana muda kabisa.......
Nakumbuka hata ule mkataba pale bandarini alishiriki utiwaji saini baadae akaja kugundua aliingizwa cha kike
Lakini Rais Samia anahitaji kushauriwa zaidi kabla ya kusaini mikataba ni lazima tuangalie mbele na tujiulize je viwanda vyetu na huo uchumi wa viwanda tutafika kweli?
Rais Samia lazima awe makini kwa watu wake wanao mshauri!