Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.
Ushindani na the best in the industry ndiyo kitu bora kuliko kubakia tunashindana na the weakest. Haijalishi leo tuna vichache vya kuuza huko kama Majani ya chai na Kahawa ila tukiwa na akili ya kuona mbele tunaweza tuka export holticulture products, nyama za mbuzi na kondoo na live animals kama mijusi, vipepeo, vinyonga etc

Kwa mtazamo wangu Mama anaupiga mwingi, tumuunge mkono tu kwa kuzalisha vilivyo bora.

Lakini kama tumeamua kuwa wasindikizaji kwenye uchumi wa Dunia basi tuendelee kubeza juhudi za Rais SSH
 
Tupambane, tuache uvivu watu wafanye Kazi. Kuna mazao mengi Sana ambayo tunaweza kuuza ulaya. Mfano mzuri ni asali yanahitajika sana Ulaya.Tuna mapori mengi Sana lakini tumeshindwa kupambana tunabaki kulaumu kwamba hatuna Cha kuuza ulaya. Ukienda pale Vijibweni watu wanazalisha asali, sisi tunabaki kulaumu.
 

Lakini hatuhitaji EPA ili tuweze kuuza hao mazao na asali Ulaya, sasa hivi bado tunapewa upendeleo kama ldc countries kuuza hayo mazao yote ulioyataja EU, hivyo kwetu EPA hatuihitaji, isitoshe kama mpaka sasa hivi hatujaweza kuuza hiyo asali EU ambapo tunapewa upendeleo maalumu tutawezaje kuuza baada ya EPA ?

Kama mtu haujajipanga siyo dhambi kusubiri kwanza kuliko kuingia kwenye mpambano ambao umeshashindwa tangia mwanzo.
 

Unajua ni kwa nini Kampuni za Bia Tanzania zinanunua shairi kutoka nje wakati inalimwa hapa hapa pia ingawaje hiyo shairi ya kutoka nje bado inatozwa kodi lkn Kampuni za bia kwao bado ni bora kuagiza nje ? Tanesco tu wanaagiza nguzo za umeme nje miti ipo unajua ni kwa nini ? Sukari ya nje pamoja na kodi bado ni rahisi klk ya hapa hapa kwetu unajua ni kwa nini ? Leo hii ukiondoa kodi hali itakuwaje ?
 
Mshauri wake ni tony blair ambaye alikuwa mpiga debe mkubwa wa epa
 
Huko tuendako nadhani nafasi ya u Makamu wa Rais itatiliwa maanani

Hiyo kansa ya kupata viongozi wabovu tayari imeshamea. Kumbuka wakati wa kumtafuta makamu wa rais, vikao vyote rais huyu anakuwepo. Hamuwezi kumchagua makamu wa rais makini kwa kusema kuuepuka tatizo la kuwa na rais kama huyu. Na kwa mifumo yetu viongozi wetu wengi ni watu wenye uwezo mdogo, lakini ni mahodari wa fitina, majungu na hila. Watu wenye uwezo huwa hawataki uongozi, maana huwa wanaogopa changamoto za kuchafuliwa kwenye uga wa siasa.
 

Umewaza kama mimi, East Africa tunawaogopa wakenya ooh wakija kwetu watachukua ajira zetu. Kwanini tusiwaze kuwa waje tushindane nao tupate kilicho bora.
Kama tunauziwa majuice famba tukomae nayo badala ya kuwapa ushindani watengeneze nzuri?
 
Kwa gharama ya Viwanda vyetu ? Vipi kuhusu ajira za watu wetu waliojiriwa kwenye hivi viwanda vyetu? Vipi kuhusu mapato ya kodi tunayoyapata sasa hivi kwa kutoza kodi imports ? Nani atafidia hiyo yote ?

Viwanda vitengeneze bidhaa bora
 

Huyo JPM sio reference ya taifa. Sio kila alichosema tufuate mama anaakili zake acha aongoze kivyake
 
Tunalima korosho,kahawa,pamba nk.

Kwa hiyo unaona ni sahihi kwa Nchi kuendelea kuwa chanzo cha mali ghafi kwa viwanda vya Ulaya! Tena wanunue kwa bei watakayo ipanga wao! Halafu wenyewe wakuletee mitumba ununue kwa bei kubwa!
 
EPA imejadiliwa toka enzi za Mkapa, hatua za mwisho hapa nilisikia tunafanya majadiliano ya mwisho kwa mambo ambayo tulikuwa hatujakubaliana, nadhani sasa tumefikia muafaka ndio maana Rais kasaini.
 
"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber" - Plato
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…