Rais Samia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa

Rais Samia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,441
Reaction score
1,050
W2 (1).jpg

Rais Samia Suluhu Hassan kushiriki
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na dirisha la Maendeleo la Kimataifa.

RAIS Samia Suluhu Hassan yuko nchini Senegal kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Kimataifa (IDA20), Mkutano huu utawezesha nchi ya Tanzania kuendelea kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania.

Mkutano huo utazingatia maeneo matano ya kipaumbele kama vile mageuzi ya Kiuchumi, Kilimo, Mifugo na Usalama wa Chakula; Mtaji wa watu; Ubunifu wa kidigitali na kiteknolojia; na mpito wa Nishati.

Kwa kuangalia ajenda za mkutano huo basi ni dhairi kuwa Tanzania itanufaika sana na uwepo wa Mhe Rais katika mkutano huo, ukizingatia ajenda zote zinashaina na maono ya Mhe Rais katika uongozi wake, ukianzia Kilimo, Nishati, Teknolojia n.k. hivyo ushiriki wake utafaidisha Tanzania kama ifuatavyo

Ushiriki wake katika mikutano hiyo ni fursa adhimu kwa Tanzania kuendelea kupenya katika ajenda ya maendeleo ya taifa, hasa katika kupata mikopo yenye masharti nafuu na ruzuku kutoka kwa mashirika ya kimataifa.

Kupitia mkutano huu wa kilele, viongozi wa Afrika wanaweza kujadili na kuona kile wanachopaswa kukisimamia, kwenye meza za majadiliano na wafadhili na washirika wa maendeleo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

Vilevile kupanua mtandao wa washirika wa maendeleo pamoja na fursa za masoko zinazopatikana nchini
Rais Samia Suluhu Hassan anapigana vita vya Kiuchumi hakika anaviweza na tuendelee kumpa moyo.
 
Back
Top Bottom