Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililoandaliwa na Baraza la Wanawake (Bawacha) wa chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, Machi 05, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema Rais Samia amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo litakalofanyika Machi 08 Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Kongamano hili la siku ya wanawake duniani ni la wanawake wote, lakini hapa Tanzania, Bawacha wamekuwa wakiliandaa kwa mafanikio makubwa kila mwaka na wamekuwa wakitoa hotuba zenye jumbe mbalimbali zinazowahusu wanawake wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Napenda kuwatangazia kuwa Rais Samia ambaye nilikuwa na mazungumzo naye jana Jumamosi, amekubali kuwa mgeni Rasmi siku hiyo na mimi nitampokea mjini Moshi siku hiyo,” alisema Mbowe

Rais Samia kukubali kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano linaloandaliwa na chama kikuu cha upinzani ni matunda ya maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kufanywa na chama chake (CCM) na Chadema.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWAPUNGIA WAJUMBE KWENYE MOJA YA MIKUTANO YA CHAMA CHAKE (CCM) AMBAPO YEYE NI MWENYEKITI TAIFA
Maridhiano hayo awali yalianza baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuishauri serikali kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Lakini maridhiano yalitiwa chachu baada ya kikao cha kwanza kati ya Rais Samia na Mbowe kukutana Ikulu, Machi 04, 2022 siku ambayo Mbowe alitoka gerezani baada ya Serikali kuifuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa huyo.

Kati ya mambo ambayo Chadema waliyapeleka kwa Rais na kutaka yarekebishwe haraka ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa wa Chadema, jambo ambalo kwa asilimia kubwa limeshafanyika.

Jambo la pili ni kuweka usalama kwa wakimbizi wa kisiasa waliokimbia nchi. Tayari viongozi wa Chadema waliokimbia nchi wamesharejea. Viongozi hao ni Tundu Lissu, Ezekia Wenje na Godbles Lema.

Jambo la tatu lililodaiwa na Chadema ni kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ambapo tayari Januari mwaka huu, Rais Samia ameondoa zuio hilo.

Jambo la nne ni upatikanaji wa Katiba mpya ambapo mpaka sasa mchakato haujaanza.

View attachment 2538065
Kwenye hili Mbowe angewaacha Mwenyekiti na Katibu Mkuu watambe kwenye siku yao. Wasiigeuze hiyo siku kuwa ya Chadema ( high table kujaa wanaume wenzake) na sio ya Bawacha. Ampokee Mwenyekiti mwenzake halafu amuache aselebuke na wanawake wenzake. Atajijengea heshima akikubali kufunikwa na wanawake kwenye siku yao.

Amandla...
 
Hii ndiyo njia JPM alitakiwa kuitumia Kuiua CHADEMA na si ile aliyoitumia!

Ni swala la Muda tu, watanzania wataamua watakavyo pigia chama gani katika uchaguzi Mkuu!

Maisha yanakwenda kwa kasi sana!
kwa taarifa yako watanzania wengi wamepuuza kitu kiitwacho uchaguzi. Tegemea kuona idadi ndogo sana ya wapiga kura chaguzi zijazo.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililoandaliwa na Baraza la Wanawake (Bawacha) wa chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, Machi 05, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema Rais Samia amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo litakalofanyika Machi 08 Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Kongamano hili la siku ya wanawake duniani ni la wanawake wote, lakini hapa Tanzania, Bawacha wamekuwa wakiliandaa kwa mafanikio makubwa kila mwaka na wamekuwa wakitoa hotuba zenye jumbe mbalimbali zinazowahusu wanawake wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Napenda kuwatangazia kuwa Rais Samia ambaye nilikuwa na mazungumzo naye jana Jumamosi, amekubali kuwa mgeni Rasmi siku hiyo na mimi nitampokea mjini Moshi siku hiyo,” alisema Mbowe

Rais Samia kukubali kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano linaloandaliwa na chama kikuu cha upinzani ni matunda ya maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kufanywa na chama chake (CCM) na Chadema.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWAPUNGIA WAJUMBE KWENYE MOJA YA MIKUTANO YA CHAMA CHAKE (CCM) AMBAPO YEYE NI MWENYEKITI TAIFA
Maridhiano hayo awali yalianza baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuishauri serikali kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Lakini maridhiano yalitiwa chachu baada ya kikao cha kwanza kati ya Rais Samia na Mbowe kukutana Ikulu, Machi 04, 2022 siku ambayo Mbowe alitoka gerezani baada ya Serikali kuifuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa huyo.

Kati ya mambo ambayo Chadema waliyapeleka kwa Rais na kutaka yarekebishwe haraka ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa wa Chadema, jambo ambalo kwa asilimia kubwa limeshafanyika.

Jambo la pili ni kuweka usalama kwa wakimbizi wa kisiasa waliokimbia nchi. Tayari viongozi wa Chadema waliokimbia nchi wamesharejea. Viongozi hao ni Tundu Lissu, Ezekia Wenje na Godbles Lema.

Jambo la tatu lililodaiwa na Chadema ni kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ambapo tayari Januari mwaka huu, Rais Samia ameondoa zuio hilo.

Jambo la nne ni upatikanaji wa Katiba mpya ambapo mpaka sasa mchakato haujaanza.

View attachment 2538065
Umoja wa Wanawake wa Chama Kingine Wao wako busy tu Kugombania Mabwana za Watu na Kurogana ili Teuzi ziwakute Wao tu.
 
Hakuna chama Cha upinzani,hapa ndipo tunapokosea na huenda ni kutokana na kasoro zilizoko kwenye lugha yetu ya kiswahili.., ukiangalia lugha ya kiingereza Huwa Wanatumia neno critical/critics, wakitaka kurejelea upinzani.., upinzani ni neno lenye ukakasi na linaloleta taswira mbaya,na huenda ndio maana viongozi wengi wa kisiasa hasa Africa wanalichukulia kama lilivyo na kutreat accordingly!
Nini maana ya opposition katika tafasiri ya lugha ya kiswahili ?
 
Hoi nimeilewa sana kwakweli, nikiwa kama mtanzania mwenye kupenda kuona tunaishi kama ndugu hili ni Heko sana
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana akina Mbowe na genge lake.
Siasa za kishamba za jiwe kwa sasa hazina nafasi,najua wafuasi wake mnaumia sana.
 
Kuna chama cha upinzani kinajiua chenyewe bila kujua.
Duh.
Kama huwezi kuwashinda basi ungana nao tu utawashinda.
 
Sukuma gang hii taarifa kwao ni msumali wa moto...povu lazima liwatoke [emoji23][emoji23][emoji854]
FB_IMG_16762806455838775.jpg
FB_IMG_16751504591944234.jpg
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana akina Mbowe na genge lake.
Sitashangaa kwenye hilo kongamano akaingilia mhimili wa Bunge. Ujue mhimili wa Mahakama tayari. Yote ni kuhakikisha kila kiumbe nchi hii kinashiriki kufuta legacy ya JPM. But will they make it? Juzi nilipita daraja la Wami my goodness. Kila binadamu alisimama kumkumbuka JPM. Hawa watu wana kazi isiyodirikika
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana akina Mbowe na genge lake.
Mnavyopenda vita na machafuko chadema mmeumbuka
 
Hakuna chama Cha upinzani,hapa ndipo tunapokosea na huenda ni kutokana na kasoro zilizoko kwenye lugha yetu ya kiswahili.., ukiangalia lugha ya kiingereza Huwa Wanatumia neno critical/critics, wakitaka kurejelea upinzani.., upinzani ni neno lenye ukakasi na linaloleta taswira mbaya,na huenda ndio maana viongozi wengi wa kisiasa hasa Africa wanalichukulia kama lilivyo na kutreat accordingly!
Neno sahihi ni USHINDANI
 
Naiona serikali ya mseto kwa siku za usooni.

Mbowe Waziri Mkuu

Tundu Lissu Waziri wa Sheria

Godblesss Lema Waziri wa Mambo ya Ndani

Hao ni kwa uchache.

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni kabla ya 2025.

Serikali tatu znakuja.

Hata hivyo, Mama awe makini sana CCM hawapendi haya mambo.

Wanasiasa wa upinzani watalazimika kuunda serikali moja na CCM Kama njia ya rahisi ya kupunguza nguvu za dola za CCM na pia ni kwasababu watanzania wamekuwa waoga kupambana na dola kuindoa CCM madarakani

Mtanielewa yakitimia.

Nimemaliza.
SIDHANI, MAANA CCM WANAVITAKA VYEO HIVYO NA NDIO UTAKUWA MWISHO WA CCM NA KUGAWANYIKA, HWAWEZI KUBALI KITU KAMA HICHO. UMEKWENDA MBALI MNO........
 
Hii ndiyo njia JPM alitakiwa kuitumia Kuiua CHADEMA na si ile aliyoitumia!

Ni swala la Muda tu, watanzania wataamua watakavyo pigia chama gani katika uchaguzi Mkuu!

Maisha yanakwenda kwa kasi sana!
Siasa ni nini? Ni kama kutongoza chama ni kijana wa kiume serikali ni wakike .ukitaka akukubali tumia ushawishi sio kumteka mwenzio anaetongoza kumtupa jela kisa kakako polisi .
 
Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?
You have a point on this aspect!
 
Mama Samia anaenda kuweka historia tangu nchi ipate uhuru kuwa ni rais wa kwanza mwanamke lakini ni rais mwenye viwangu vya juu vya hekima na busara. Uongozi ni kipaji lakini hekima na busara mama Samia ana kipaji Cha uongozi.
 
Back
Top Bottom