Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Dr Slaa amesema leo kama haya anayofanya Rais hawakukubaliama kwenye Kamati Kuu ya CCM basi leo kuna watu watalala na viatu na wengine watalazwa hospitalini.
Sipati picha ya Mkumbo na Mtaturu leo wana hali gani huko walipo
 
Naiona serikali ya mseto kwa siku za usooni.

Mbowe Waziri Mkuu

Tundu Lissu Waziri wa Sheria


Godblesss Lema Waziri wa Mambo ya Ndani

Hao ni kwa uchache.

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni kabla ya 2025.

Serikali tatu znakuja.

Hata hivyo, Mama awe makini sana CCM hawapendi haya mambo.

Wanasiasa wa upinzani watalazimika kuunda serikali moja na CCM Kama njia ya rahisi ya kupunguza nguvu za dola za CCM na pia ni kwasababu watanzania wamekuwa waoga kupambana na dola kuindoa CCM madarakani

Mtanielewa yakitimia.

Nimemaliza.
Ndugu, serikali ya mseto si jambo jema kwa wapenda democrasia. Upinzani ni lazima uwepo kuleta fikra mbadala.
 
Kwa hivyo watanzania hawataipigia kura CHADEMA kisa imemwalika rais wa nchi kwenye mkutano wa BAWACHA?. Wakati CHADEMA wanalimwa risasi na kesi za m hongo hao wananchi walikuwa wapi?, Acha kuwasingizia wananchi kwa Jambo ambalo sio lao.
Unamakasiriko mengi sana!

Soma ukiwa umetulia!

Si kila uzi ni kulialia!

Kunanyakati inatubidi tufikirie zaidi ya milengo yetu ya kisiasa!

Unanilisha maneno. Tujipe Muda mkuu wangu!

Muda ni mwamuzi wa Khaki!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililoandaliwa na Baraza la Wanawake (Bawacha) wa chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, Machi 05, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema Rais Samia amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo litakalofanyika Machi 08 Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Kongamano hili la siku ya wanawake duniani ni la wanawake wote, lakini hapa Tanzania, Bawacha wamekuwa wakiliandaa kwa mafanikio makubwa kila mwaka na wamekuwa wakitoa hotuba zenye jumbe mbalimbali zinazowahusu wanawake wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Napenda kuwatangazia kuwa Rais Samia ambaye nilikuwa na mazungumzo naye jana Jumamosi, amekubali kuwa mgeni Rasmi siku hiyo na mimi nitampokea mjini Moshi siku hiyo,” alisema Mbowe

Rais Samia kukubali kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano linaloandaliwa na chama kikuu cha upinzani ni matunda ya maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kufanywa na chama chake (CCM) na Chadema.


RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWAPUNGIA WAJUMBE KWENYE MOJA YA MIKUTANO YA CHAMA CHAKE (CCM) AMBAPO YEYE NI MWENYEKITI TAIFA
Maridhiano hayo awali yalianza baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuishauri serikali kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Lakini maridhiano yalitiwa chachu baada ya kikao cha kwanza kati ya Rais Samia na Mbowe kukutana Ikulu, Machi 04, 2022 siku ambayo Mbowe alitoka gerezani baada ya Serikali kuifuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa huyo.

Kati ya mambo ambayo Chadema waliyapeleka kwa Rais na kutaka yarekebishwe haraka ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa wa Chadema, jambo ambalo kwa asilimia kubwa limeshafanyika.

Jambo la pili ni kuweka usalama kwa wakimbizi wa kisiasa waliokimbia nchi. Tayari viongozi wa Chadema waliokimbia nchi wamesharejea. Viongozi hao ni Tundu Lissu, Ezekia Wenje na Godbles Lema.

Jambo la tatu lililodaiwa na Chadema ni kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ambapo tayari Januari mwaka huu, Rais Samia ameondoa zuio hilo.

Jambo la nne ni upatikanaji wa Katiba mpya ambapo mpaka sasa mchakato haujaanza.

View attachment 2538065
I'm feeling very proud of my president.
Long live our kind president.
God be with you.
 
Kwa nchi zenye demokrasia changa kama ya kwetu ni hatari sana air.tel na voda.com kufanya kazi kwa kushirikiana, ofisi ya c.ag na taasisi za seri,kali, mara nyingi kwenye kushirikiana kwa namna hiyo, mwananchi wa kawaida hana chake.

Would never condone siasa za hatari za aina ya akina mako.nda, sa,baya, lis.su, ali ,hapi, kheri ja.mes etc lakini naamini ushirikiano wa kiasi hiki kati ya cha..dema na cc,m hauwezi kuwa na afya kwa ustawi wa n.chi, hawa wanashirikiana kula.
Muda utaongea

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Chadema tulikipenda ila CCM imekipenda zaidi.!
 
Kwa nchi zenye demokrasia changa kama ya kwetu ni hatari sana air.tel na voda.com kufanya kazi kwa kushirikiana, ofisi ya cag na taasisi za serikali, mara nyingi kwenye kushirikiana kwa namna hiyo, mwananchi wa kawaida hana chake.

Would never condone siasa za hatari za aina ya akina makonda, sabaya, lissu, ali hapi, kheri james etc lakini naamini ushirikiano wa kiasi hiki kati ya chadema na ccm hauwezi kuwa na afya kwa ustawi wa nchi, hawa wanashirikiana kula.
Muda utaongea

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Kajinyonge wewe huna faida kwa taifa letu na wewe ni adui mkubwa wa umoja wetu
 
Hii ndiyo njia JPM alitakiwa kuitumia Kuiua CHADEMA na si ile aliyoitumia!

Ni swala la Muda tu, watanzania wataamua watakavyo pigia chama gani katika uchaguzi Mkuu!

Maisha yanakwenda kwa kasi sana!
Coment yako imenifikirisha sana, kwamba Samia ameua Upinzani bila kutumia nguvu nyingi...
 
Coment yako imenifikirisha sana, kwamba Samia ameua Upinzani bila kutumia nguvu nyingi...
Hakuna chama Cha upinzani,hapa ndipo tunapokosea na huenda ni kutokana na kasoro zilizoko kwenye lugha yetu ya kiswahili.., ukiangalia lugha ya kiingereza Huwa Wanatumia neno critical/critics, wakitaka kurejelea upinzani.., upinzani ni neno lenye ukakasi na linaloleta taswira mbaya,na huenda ndio maana viongozi wengi wa kisiasa hasa Africa wanalichukulia kama lilivyo na kutreat accordingly!
 
Hii ndo dini ya mnyazi mungu tunataka muslimu ili msije ikosa Pepo. Ukifa mkristo unaingia motoni mojakwamoja ndo mana Huwa tunataka msiende huko
Imeandikwa "USIMJIBU MPUMBAVU SAWASAWA NA UPUMBAVU WAKE, USIJE UKAFANANA NAE"
 
Back
Top Bottom