Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Coment yako imenifikirisha sana, kwamba Samia ameua Upinzani bila kutumia nguvu nyingi...

Ni upinzani wenyewe wamejipeleka na kujipendekeza kwa Rais.

Sidhani kama Samia anastahili credit ya kubuni namna ya kuua upinzani. Wenyewe wana commit suicide.
 
Maccm ndiyo wanahitaji kutumia jina hilo ili kuwafanya wananchi wazidi kuwachukia vyama mbadala
 
Umesahahu jiwe alikuwa anaweka jiwe hadi kwenye masoko ya kuuzia mchicha?

Kwanini hakuwaachia watendaji waliochini yake?

Mbowe anaenda pale kumpokea kiongozi mwenzake wa ngazi za juu kabisa wa nchi yetu
 
kwa taarifa yako watanzania wengi wamepuuza kitu kiitwacho uchaguzi. Tegemea kuona idadi ndogo sana ya wapiga kura chaguzi zijazo.
Wawaulize wa [emoji1184] jinsi watu walivyo susia uchaguzi wao
 

Mbona kibuyu kilimalizwa zamani na akina Palamagamba Kabudi , Lukuvi na Sukuma Gang
 
Tuunde na serikali ya umoja wa kitaifa,au unapochagua viongozi siyo lazima wawe wa chama chako!! Ila viongozi wanaoshabikia ushoga hao tu ndiyo hapana .
Unamchagua mwanachama mwenzio kumbe bogus wakati kwenye vyama vingine wako jiniasi wachapakazi.

Hili la vyama kushirikiana ni zuri sana .Kwa Hilo nampa Mh Rais kongole.
Let us build the together our nation !!
 
Samia apewe PhD ya heshima ya Siasa.
Sasa yule shetani wenu alishindwa Nini mambo kama haya? Hakuna haja ya kutumia nguvu kwenye siasa ni consensus tu na win-win situation.

Mbona Kenyatta na Odinga walikua rivals ila wakafanya handshake na hukuona vurugu tokea hapo. Upinzani sio uadui sijui nani alituaminisha hili mnaweza mkashindana bila kugombana.
 
Mnajifia kisayansi sana
 
kwa taarifa yako watanzania wengi wamepuuza kitu kiitwacho uchaguzi. Tegemea kuona idadi ndogo sana ya wapiga kura chaguzi zijazo.
Si mmeridhiana? Sasa mtasusiaje uchaguzi?
 
Umesahahu jiwe alikuwa anaweka jiwe hadi kwenye masoko ya kuuzia mchicha?

Kwanini hakuwaachia watendaji waliochini yake?

Mbowe anaenda pale kumpokea kiongozi mwenzake wa ngazi za juu kabisa wa nchi yetu
Nisome vizuri Mkuu. Sijakataa Mbowe kumpokea Mwenyekiti mwenzake. Nilichosema ni kuwa mkutano wa wakina mama ni lazima uwe na sura ya wakina mama. Itakuwa vyema kama mara baada ya kumpokea Mwenyekiti mwenzake amuachie meza Mwenyekiti wa Bawacha ambae sio tu ni mwanamke lakini ni mzanzibari kama Mwenyekiti wa CCM. Haitapendeza kama meza kuu watajazwa wakina Lema, Heche, Msigwa na kuwaacha wakina Suzan na wanawake waandamizi kibao wa Bawacha. Ingekuwa mimi wale wakina mama waliojigalagala pale kwenye ubalozi wa Marekani, waliofungwa, yule wa Chato, kuna yule wa Njombe n.k. wotewangepewa nafasi za kipekee. Chadema inatakiwa kuwashukuru kwa jinsi walikipigania chama chao. Wanaume tunawaona katika kila mkutano. Tarehe 8 ni siku ya wanawake wa Bawacha kutamba. Wasipokonywe siku hiyo.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…