Nimependa kusikia kwamba Watanzania sasa wanaishi kama ndugu na wanashirikiana.
Watanzania miaka yote tumekaa pamoja kwenye familia, kwenye mahusiano, kanisani, kazini na maeneo mbalimbali yanayotuleta pamoja.
Lakini Watanzania hao hao tumekuwa maadui kwenye ulingo wa siasa. Maana yake tunaelewana na kusema NI ndugu kwenye kila kitu Ila inapokuja kwenye siasa tunafanya unafiki kwamba Sisi siyo ndugu.
Naamini makubaliano ya Mbowe na Mhe. Rais kuhusu Rais kuwa mgeni rasmi siku ya wanawake yamepokelewa Kwa mtizamo tofauti. Nini maoni yako?
Maoni yangu Mimi NI haya;
Mhe. Rais kuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano wa chadema nikutuma salamu Kwa vyombo vya dola kwamba Tanzania sasa NI moja. Nikutuma salam Kwa viongozi Aina ya Muro, Makonda, Mnyeti, Gambo, Nape, Mwigulu, Ndugai, Mkumbo, Molel, Tulia, Bashiru, Kabudi, Lukuvi, nk kwamba siyo lazima uwe na roho ya kikatili Ndipo ukubalike au uongoze....Duniani tunapita ccm au CDM tutaviacha......Sisi NI ndugu.