Rais Samia kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Kimataifa Kujadili Nishati Safi utakaofanyika Ufaransa

Na hasa tuzo hiyo ikiwa wanapewa viongozi makatili, maana huyu katimua wamasai Ngorongoro
Nani kakwambia kuwa kuna ardhi ya mtu hapa nchini. Ardhi yote ni ya umma na ipo chini ya Rais anayeilinda kwa niaba ya umma. Kwani mara ngapi unasikia eneo fulani watu wanahamishwa kupisha shughuli fulani inayogusa maslahi ya umma?

Kwa hiyo ulitaka Wamasai waendelee kukaa eneo ambalo tayari wamekuwa wengi kupita idadi inayohitajika kwa upande wa watu na mifugo yao? Kwa hiyo unataka watalii wakija nchini waje kuangalia mbuzi na watu badala ya simba ,tembo,twiga n.k. hufahamu kuwa kwa kuendelea kuwa wengi na kuzaliana kwa upande wa watu na mifugo yao ilikuwa inahatarisha uhifadhi?

Wewe unafikiri kwanini Wamasai walikubali kuhama kwa hiyari yao wenyewe? Hujuwi hata wao walitambua umuhimu wa wao kuondoka eneo hilo ambalo tayari walikuwa wameongezeka zaidi ukilinganisha na idadi inayohitajika?
 
ni rais yupo wa tanzania alishapata hizo tuzo?
Mbona imeuliza swali la kitoto sana ambalo hakiendani na hadhi yako. Kwa hiyo kama hakuna aliyepata ndio jibu kwamba Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mama Samia Hawezi kupata? Au hoja yako ni ipi ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo
 
Analo la kuchangia huyu? Au atakuwepo kimwili tu?
Uwe na adabu kwa mamlaka. Unafikiri Dunia ni wajinga waliotambua uwezo wake mkubwa kiakili? Dunia inatambua maono makubwa aliyonayo na yeye ndiye ameionyesha njia Dunia na kuipa msukumo wa kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia .kwa kutunga sera na sheria zitakazo chochea matumizi makubwa ya nishati hiyo safi kwa ajili ya kupikia.
 
Machawa muwe mnakubaliana nani anapost mada ipi.

Maana wote mnakua kama mnashindana nani atatangulia kupost.
Presha itakuuwa na wivu wako uliokujaa kifuani pako kwa mafanikio makubwa ya Mheshimiwa Rais.
 
Na kwamba imeelekezwa Wauziwe Waarabu au siyo?
 
Tutaanika kila kitu
Sipendagi mtu wa kupiga blaa blaa na porojo. Weka huo ushahidi wa mkataba wa mauziano. CHADEMA mmeshakuwa matapeli na madalali wa kisiasa ndio maana midomo yenu inafanya kazi ya kuropoka,kuzusha ,kuhemuka na kutunga uongo uongo tu usio na mashiko. Ndio maana mnaendelea kupuuzwa na watanzania.
 
Kadco inazungumzwa hadi bungeni kuuziwa KIA na majirani zake nayo hujui? tena bunge la chama kimoja, Utakuwa umelogwa sana!
 
Huwezi ukaelewa kwa kuwa umeshapofuka akili yako.
Samia atabakia kupewa zile PhD zake na waarabu , wahindi na waturuki huku akiwagawia mbuga za wanyama, mapori ya akiba na bandari kwa bei ya kutupa !

Hizo tuzo unazoota apewe utaendelea kuota hadi Samia ataanza kutembelea mkongojo.
 
Pamoja na kua mwenyekti asijefungwa na mbinu za kuzizuia nchi zetu kuwekeza na kuendeleza nishati kama makaa ya mawe na petroli. Hawa wenzetu wa magharibi ni wajanja . Wao baada ya kuchafua mazingira wanataka hatua za kutuzuia nchi zingine kutumia nishati ambazo tunazo kisha tuwe wateja wao wa mashine na mitambo ya nishati wanazotaka kuendeleza wao huku wakihakikisha tunabakia wateja na wasindikizaji na watumishi wao watiifu. Wanampa mama uenyekiti ili tukikange kwa mafuta yetu wenyewe. Mama anahitaji kuambatana na wataalaam wazalendo wenye ujuzi sio watu kama kina kina kipara.
 
Samia atabakia kupewa zile PhD zake na waarabu , wahindi na waturuki huku akiwagawia mbuga za wanyama, mapori ya akiba na bandari kwa bei ya kutupa !

Hizo tuzo unazoota apewe utaendelea kuota hadi Samia ataanza kutembelea mkongojo.
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais na uache chuki yako binafsi kwa Mama yetu. Uwezo wa kiakili huwezi ukaufikia wewe na watu wenye akili finyu aina yako. Dunia nzima inatambua uwezo wake mkubwa kiakili ndio maana Inaendelea kumpa heshima na kumpa nafasi ya kutoa Elimu na kupata hekima ,busara na maarifa makubwa aliyonayo.
 
Acha wivu wako wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…