Rais Samia kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Kimataifa Kujadili Nishati Safi utakaofanyika Ufaransa

Rais Samia kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Kimataifa Kujadili Nishati Safi utakaofanyika Ufaransa

Na hasa tuzo hiyo ikiwa wanapewa viongozi makatili, maana huyu katimua wamasai Ngorongoro
Nani kakwambia kuwa kuna ardhi ya mtu hapa nchini. Ardhi yote ni ya umma na ipo chini ya Rais anayeilinda kwa niaba ya umma. Kwani mara ngapi unasikia eneo fulani watu wanahamishwa kupisha shughuli fulani inayogusa maslahi ya umma?

Kwa hiyo ulitaka Wamasai waendelee kukaa eneo ambalo tayari wamekuwa wengi kupita idadi inayohitajika kwa upande wa watu na mifugo yao? Kwa hiyo unataka watalii wakija nchini waje kuangalia mbuzi na watu badala ya simba ,tembo,twiga n.k. hufahamu kuwa kwa kuendelea kuwa wengi na kuzaliana kwa upande wa watu na mifugo yao ilikuwa inahatarisha uhifadhi?

Wewe unafikiri kwanini Wamasai walikubali kuhama kwa hiyari yao wenyewe? Hujuwi hata wao walitambua umuhimu wa wao kuondoka eneo hilo ambalo tayari walikuwa wameongezeka zaidi ukilinganisha na idadi inayohitajika?
 
ni rais yupo wa tanzania alishapata hizo tuzo?
Mbona imeuliza swali la kitoto sana ambalo hakiendani na hadhi yako. Kwa hiyo kama hakuna aliyepata ndio jibu kwamba Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mama Samia Hawezi kupata? Au hoja yako ni ipi ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo
 
Analo la kuchangia huyu? Au atakuwepo kimwili tu?
Uwe na adabu kwa mamlaka. Unafikiri Dunia ni wajinga waliotambua uwezo wake mkubwa kiakili? Dunia inatambua maono makubwa aliyonayo na yeye ndiye ameionyesha njia Dunia na kuipa msukumo wa kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia .kwa kutunga sera na sheria zitakazo chochea matumizi makubwa ya nishati hiyo safi kwa ajili ya kupikia.
 
Machawa muwe mnakubaliana nani anapost mada ipi.

Maana wote mnakua kama mnashindana nani atatangulia kupost.
Presha itakuuwa na wivu wako uliokujaa kifuani pako kwa mafanikio makubwa ya Mheshimiwa Rais.
 
Nani kakwambia kuwa kuna ardhi ya mtu hapa nchini. Ardhi yote ni ya umma na ipo chini ya Rais anayeilinda kwa niaba ya umma. Kwa mara ngapi unasikia eneo fulani watu wanahamishwa kupisha shgt fulani inayoguswa maslahi ya umma?

Kwa hiyo ulitaka Wamasai waendelee kukaa eneo ambalo tayari wamekuwa wengi kupita idadi inayohitajika kwa upande wa watu na mifugo yao? Kwa hiyo unataka watalii wakija wake kuangalia mbuzi na watu badala ya simba ,tembo,twiga n.k. hufahamu kuwa kwa kuendelea kuwa wengi na kuzaliana ilikuwa inahatarisha uhifadhi.

Wewe unafikiri kwanini Wamasai walikubali kuhama kwa hiyari yao wenyewe? Hujuwi hata wao walitambua umuhimu wa wao kuondoka eneo hilo ambalo tayari walikuwa wameongezeka zaidi ukilinganisha na idadi inayohitajika?
Na kwamba imeelekezwa Wauziwe Waarabu au siyo?
 
Tutaanika kila kitu
Sipendagi mtu wa kupiga blaa blaa na porojo. Weka huo ushahidi wa mkataba wa mauziano. CHADEMA mmeshakuwa matapeli na madalali wa kisiasa ndio maana midomo yenu inafanya kazi ya kuropoka,kuzusha ,kuhemuka na kutunga uongo uongo tu usio na mashiko. Ndio maana mnaendelea kupuuzwa na watanzania.
 
Sipendagi mtu wa kupiga blaa blaa na porojo. Weka huo ushahidi wa mkataba wa mauziano. CHADEMA mmeshakuwa matapeli na madalali wa kisiasa ndio maana midomo yenu inafanya kazi ya kuropoka,kuzusha ,kuhemuka na kutunga uongo uongo tu usio na mashiko. Ndio maana mnaendelea kupuuzwa na watanzania.
Kadco inazungumzwa hadi bungeni kuuziwa KIA na majirani zake nayo hujui? tena bunge la chama kimoja, Utakuwa umelogwa sana!
 
Huwezi ukaelewa kwa kuwa umeshapofuka akili yako.
Samia atabakia kupewa zile PhD zake na waarabu , wahindi na waturuki huku akiwagawia mbuga za wanyama, mapori ya akiba na bandari kwa bei ya kutupa !

Hizo tuzo unazoota apewe utaendelea kuota hadi Samia ataanza kutembelea mkongojo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa mara nyingine tena Dunia imempatia heshima ya kipekee kabisa na ya hadhi ya juu kabisa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa nishati safi ya kupikia na kuwa Mwenyekiti Mwenza wa mkutano huo.

Rais wetu amepewa heshima hiyo ya kipekee kabisa kutokana kutambua mchango wake chanya na juhudi zake kubwa za kuhakikisha kuwa Dunia inaelekeza nguvu zake zote katika matumizi ya nishati safi ya kupikia .na kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, ambazo zimekuwa na athari kubwa sana kimazingira kwa kuchochea ukatwaji wa miti unaopelekea mabadiliko ya tabia ya nchi , pamoja na kuhatarisha afya za watumiaji ambapo vifo vingi sana vimekuwa vikitokea kutokana na matumizi ya nishati hizo za kuni na mkaa kila mwaka..

Katika safari hiyo itakayomfanya kuwepo nchini Ufaransa kwa siku nne ,itawakutanisha viongozi na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti tofauti Duniani.lakini pia Rais wetu mpendwa atakutana na Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Emmanueli Macron na kufanya Naye mazungumzo ikulu ya Ufaransa katika kuimarisha ushirikiano wa nchi zetu.

Katika mkutano huo mbali na masuala mbalimbali yatakayojadiliwa ,lakini pia mkutano huo utaangazia na kujikita katika kuyashawishi mataifa yaliyoendelea na taasisi za kifedha kutoa ahadi ya fedha na kubadili sera na sheria zitakazo chochea matumizi ya nishati safi na salama,kutunga sera zitakazorahisisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

Ikumbukwe pia kuwa hapa nchini Mheshimiwa Rais ameshaanza kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa nishati safi ya kupikia inaanza kutumika kwa taasisi zote zinazohudumia watu wengi, kama vile kwenye kambi za jeshi,vyuo n.k.lakini pia wadau wamekuwa wakishauri pia serikali iangalie namna ya kupunguza au kuondoa kodi kabisa katika uagizaji wa majiko ya gas ili yauzwe kwa bei ya chini na kumfanya mwananchi Amudu gharama za kununua na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni.

Lakini pia wengine wametaka kuwa serikali iangalie namna ya kuweka sera nzuri ambazo zitapelekea ujazaji wa gas kushuka na ikiwezekana mtungi mdogo ujazwe gas na mwananchi walau hata kwa shilingi elfu kumi au kama itazidi basi isizidi shilingi elfu kumi na tano. Jambo ambalo serikali yetu imesema lengo ni kumfanya kila mtanzania atumie nishati safi ya kupikia na tayari imeweka mikakati ya kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa bei ndogo kabisa ambayo kila mtu ataimudu na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Tumuombee Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu asafiri salama na kufika salama kabisa katika mkutano huo.lakini pia tumuombee Rais wetu ili Mungu amtie nguvu na kumpatia afya njema wakati wote awapo safarini na katika mkutano huo ambao macho na Dunia nzima yataelekezwa kwake na kumsikiliza Mama Wa Dunia akizungumza na kushusha NONDO zitakazoiteka Dunia hakuipa Elimu ya nishati safi ya kupikia hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Rais Samia Kama Mama anatambua athari za matumizi ya kuni na mkaa kiafya.

Jiulizeni kuna viongozi wangapi hapa Afrika? Kwanini apewe tu Dkt Samia heshima hiyo? Kwanini Dunia nzima ikubali na kupitisha jina lake kuwa Mwenyekiti Mwenza? Ndio muelewe watanzania wenzangu napowaambiaga kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe na kwamba kama Afrika ingekuwa nchi moja basi Mama yetu ndiye angekuwa Rais wake. Kwa hakika Mama yetu anaendelea kuliheshimisha sana Taifa letu.

Kwa sasa mtanzania unaweza kusafiri hata bila passport na watu wakasahau kukuuliza pale utakaposema wewe ni mtanzania, kwa kuwa watanzania tumeheshimishwa sana huko Duniani na kufanya tuaminike kama watu makini, waaminifu, wazalendo,akili kubwa na wenye kuiweka Dunia katika hali ya usalama zaidi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan atasafiri kwenda Nchini Ufaransa kuhudhuria na kuwa Mwenyekiti mwenza wa mkutano wa kimataifa wa nishati safi ya kupikia unaowakutanisha Wakuu wa Nchi mbalimbali duniani.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi January Makamba leo Jijini Dar es salaam, amesema Rais Samia atakuwa Nchini Ufaransa kwa siku nne kuanzia May 12 hadi May 15 ambapo Tanzania imeshirikishwa kwenye mkutano huo kutokana na jitihada kubwa zinazofanyika ndani ya Tanzania kusukuma ajenda hiyo ya kuwawezesha Watu wote kutumia nishati safi ya kupikia ili kulinda afya zao na kulinda mazingira.

“Mkutano huo una malengo matatu, kwanza kuifanya hii iwe ajenda ya kimataifa na ipate Wadau wengi zaidi, pili ni kuchukua hatua madhubuti za kisera zinazoweza kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, na tatu ni Washiriki Nchi zilizoendelea na Taasisi za Fedha za kimataifa kutoa ahadi za fedha na misaada na Nchi kutoa ahadi za kubadilisha sera na sheria ili kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akiwa Ufaransa, Dr. Samia anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Ikulu jijini Paris katika kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Nchi hizo mbili.
Pamoja na kua mwenyekti asijefungwa na mbinu za kuzizuia nchi zetu kuwekeza na kuendeleza nishati kama makaa ya mawe na petroli. Hawa wenzetu wa magharibi ni wajanja . Wao baada ya kuchafua mazingira wanataka hatua za kutuzuia nchi zingine kutumia nishati ambazo tunazo kisha tuwe wateja wao wa mashine na mitambo ya nishati wanazotaka kuendeleza wao huku wakihakikisha tunabakia wateja na wasindikizaji na watumishi wao watiifu. Wanampa mama uenyekiti ili tukikange kwa mafuta yetu wenyewe. Mama anahitaji kuambatana na wataalaam wazalendo wenye ujuzi sio watu kama kina kina kipara.
 
Samia atabakia kupewa zile PhD zake na waarabu , wahindi na waturuki huku akiwagawia mbuga za wanyama, mapori ya akiba na bandari kwa bei ya kutupa !

Hizo tuzo unazoota apewe utaendelea kuota hadi Samia ataanza kutembelea mkongojo.
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais na uache chuki yako binafsi kwa Mama yetu. Uwezo wa kiakili huwezi ukaufikia wewe na watu wenye akili finyu aina yako. Dunia nzima inatambua uwezo wake mkubwa kiakili ndio maana Inaendelea kumpa heshima na kumpa nafasi ya kutoa Elimu na kupata hekima ,busara na maarifa makubwa aliyonayo.
 
Pamoja na kua mwenyekti asijefungwa na mbinu za kuzizuia nchi zetu kuwekeza na kuendeleza nishati kama makaa ya mawe na petroli. Hawa wenzetu wa magharibi ni wajanja . Wao baada ya kuchafua mazingira wanataka hatua za kutuzuia nchi zingine kutumia nishati ambazo tunazo kisha tuwe wateja wao wa mashine na mitambo ya nishati wanazotaka kuendeleza wao huku wakihakikisha tunabakia wateja na wasindikizaji na watumishi wao watiifu. Wanampa mama uenyekiti ili tukikange kwa mafuta yetu wenyewe. Mama anahitaji kuambatana na wataalaam wazalendo wenye ujuzi sio watu kama kina kina kipara.
Acha wivu wako wewe.
 
Back
Top Bottom