Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
RAIS DKT. SAMIA KUZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA NA UANZAJI RASMI WA TRENI YA MIZIGO YA SGR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala na kuanza rasmi kwa safari za treni ya mizigo ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma itafanyika tarehe 31 Julai, 2025, Kwala, mkoani Pwani, ikihusisha pia upokeaji wa mabehewa mapya na yaliyokarabatiwa ya reli ya zamani (MGR)
Bandari Kavu ya Kwala, iliyojengwa Vigwaza, kilomita 90 kutoka Dar es Salaam, ina uwezo wa kuhudumia Makasha 823 kwa siku (takribani 339,500 kwa mwaka), sawa na asilimia 30 ya Makasha yote ya Bandari ya Dar es salaam na kueleza kuwa eneo hilo lilichaguliwa kutokana na jiografia nzuri na ardhi ya Serikali isiyo na migogoro.
Pia, Treni ya mizigo ya SGR imeanza rasmi kutoa huduma kuanzia tarehe 27 Juni, 2025 baada ya majaribio kufanyika, ambapo imepunguza muda wa kusafirisha Mizigo kutoka masaa 16 hadi masaa 4 kati ya Dar es Salaam na Dodoma na tayari makampuni kama Azania Group na Dangote Cement zimeshanufaika na huduma hiyo.
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuboresha reli ya zamani (MGR) kwa kupokea mabehewa 50 mapya na 20 yaliyokarabatiwa ili kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo nchini na kukuza uchumi.
Faida zitakazopatikana ni pamoja na Kupunguza msongamano bandarini na barabarani, Kuongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam, Kupunguza ajali gharama za usafirisaji sambamba na kukuza ajira na biashara katika Mikoa jirani