Rais Samia Kuzindua Miradi Nane Kizimkazi Day"

Rais Samia Kuzindua Miradi Nane Kizimkazi Day"

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi nane yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni moja iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni kuelekea katika Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Day) linalotarajiwa kuanza Àgosti 26 mwaka huu.

Akiota taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake Tunguu, jana, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hadid Rashid Hadid, alisema tamasha hilo linataraiwa kufunguliwa Agosti 26 mwaka huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Alieleza kuwa kilele tamasha hilo kitakuwa Agosti 31 mwaka ambapo mgeni rasmi Rais wa ¡amhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia.

Aliitaja miradi hiyo itakayofunguliwa na Rais Dk. Samia ni ufunguzi wa Tawi la Benki ya NMB Shehia ya Paje, uzinduzi wa ukumbi wa mitihani Skuli ya Sekondari Muyuni, uzinduzi wa madarasa matatu ya Skuli ya Msingi Muyuni B, uwanja wa tenesi na uzinduzi wa kwanza wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Kizimkazi.

"Miradi mengine ni uzinduzi wa huduma za mama na mtoto, uzinduzi wa huduma ya mtandao, uzinduzi wa madrasa, milango minne ya maduka pamoja na Tawi la CM Kizimkazi Mkunguni na uzinduzi wa Skuli ya Msingi Kizimkazi Mkunguni," alibainisha.

Akizungumzia miradi itakayowekewa mawe ya msingi ni mradi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Kizimkazi na
kutembelea ujenzi wa mradi wa soko la Kizimkazi Dimbani.

Alisema mbali na miradi hivo katika kuelekea siku ya kilele shughuli mbalimbali zinatarajiwa kufanywa na Rais Dk. Samia ikiwemo kutoa misaada kwa wazee kuanzia miaka 80 katika Wilaya ya Kusini, msaada kwa watoto yatima, kutembelea wagoniwa Hospitali ya Wilaya Kitogani na Makunduchi kisha kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa skuli za wilaya hiyo.

Hata hivyo, alisema Dk. Samia atahamasisha unywaji maziwa kwa wanafunzi na wananchi wa Wilaya ya Kusini na kutoa magari mawili ya kutoa huduma Kituo cha Afya Kizimkazi Dimbani na magari mawili kwa Kituo cha Polisi
Kizimkazi.
 
Kizimkazi si sawa na kijiji tu huku kwetu? Mbona miradi yote inapelekwa huko?
 
Samia Suluhu ambaye ni rais wa kurithi Tanzania baada ya kifo cha Rais Magufuli amesifu tamasha linalofanyika kijijini kwake kule Kizimkazi kwa kupongeza uwingi wa watu wanao hudhuria.

"....kwa sasa maboti yanavyojaa kutokea Bara kuja Kizimkazi hadi raha. Tudumishe tamasha hili."

rais Samia.
 
Samia Suluhu ambaye ni rais wa kurithi Tanzania baada ya kifo cha Rais Magufuli amesifu tamasha linalofanyika kijijini kwake kule Kizimkazi kwa kupongeza uwingi wa watu wanao hudhuria.

"....kwa sasa maboti yanavyojaa kutokea Bara kuja Kizimkazi hadi raha. Tudumishe tamasha hili."

rais Samia.
Anashangilia mavuno yake toka kwa ng'ombe zake wa bara.
 
Back
Top Bottom