#COVID19 Rais Samia kuzindua na kupata Chanjo ya COVID-19 Julai 28, 2021

Uharaka wa Rais wetu kuchanjwa chanjo ya UIVIKO 19 unatoka wapi? Je! Ni kutokana na masharti ya mkopo wa World Bank? Je! Ni kutokana na masharti ya mabeberu ili aonekane yupo kinyume na misimamo ya mwendazake? Je! Yeye naye ni sehemu muhimu ya kutekeleza mipango ya NWO? Je! Anafanya hivyo kwa msukumo binafsi wa kutaka kupata umaarufu mbele ya jumuiya ya kimataifa pasipo kujali athari za kiafya juu ya maamuzi yake katika siku zijazo?

Mimi bado nipo upande wa wale wanaotaka tujipe kwanza " benefit of doubt" kabla ya kuanza matumizi rasmi ya chanjo hizi. Kwa maana ktk hali ya kawaida tu huwezi kuamua kukimbilia chanjo ambazo matumizi yake yamekataliwa nchini USA na Canada, halafu leo eti zinaletwa na USA hiyo hiyo kama msaada kwa nchi yetu.
 
Chanjo gani atakayo chanjwa?
 
Uzinduzi utatumika kujibu mengi na pengine tutapashwa mpaka tupashike
 
Hivi mna nini watanzania? Wewe kuna mtu amekushikia panga uchanje kwa nguvu? Kwanini isiachwe kwa anayetaka sawa na asiyetaka sawa?
 
Ndio ku sakrifaisi maisha yake kwa ajili ya watanzania
 
Nimeamua mimi na familia yangu hakuna atakaye choma hiyo chanjo.

Azindue asizindue hainihusu.
 
achanjwe tu!, ikiwezekana na nduguze wachanjwe...sisi tupo fresh...tunajifukiza, malimao tangawizi michaichai kwa sana, ndimu vitunguu swaumu. hata ikija covid-19 ya kumi bado haitatuweza kabisaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…