#COVID19 Rais Samia kuzindua na kupata Chanjo ya COVID-19 Julai 28, 2021

#COVID19 Rais Samia kuzindua na kupata Chanjo ya COVID-19 Julai 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya uzinduzi wa zoezi la uchanjaji Jumatano asubuhi, Ikulu ya Dar es Salaam, atazindua chanjo ya corona kwa kuchanjwa yeye mwenyewe. Baada ya uzinduzi huo Wizara ya afya itaendelea na taratibu zingine za usambazaji wa chanjo hiyo.. tibu zingine za usambazaji wa chanjo hiyo.

Hili linakuja licha ya Upingaji mkubwa wa chanjo hiyo kutoka kwa Mbunge waKawe Mh Gwajima ambaye anasema Chanjo hiyo imeletwa kwa mkakati maalum wa kuwadhuru Waafrika.

Sasa tumsikilize nani sisi wananchi wa Kawe. Tumfuate Mheshimiwa Mbunge wetu ama tumfuate Rais wetu na Serikali yetu iliyokataa chanjo mwaka jana. Ama serikali imeamua kufuata wataalamu wa afya na sasa Mbunge anahujumu Serikali?

Mwisho wa yote namuasa Gwajima achunge ulimi wake, kwani nje ya mfumo yeye hana lolote.
 
Uharaka wa Rais wetu kuchanjwa chanjo ya UIVIKO 19 unatoka wapi? Je! Ni kutokana na masharti ya mkopo wa World Bank? Je! Ni kutokana na masharti ya mabeberu ili aonekane yupo kinyume na misimamo ya mwendazake? Je! Yeye naye ni sehemu muhimu ya kutekeleza mipango ya NWO? Je! Anafanya hivyo kwa msukumo binafsi wa kutaka kupata umaarufu mbele ya jumuiya ya kimataifa pasipo kujali athari za kiafya juu ya maamuzi yake katika siku zijazo?

Mimi bado nipo upande wa wale wanaotaka tujipe kwanza " benefit of doubt" kabla ya kuanza matumizi rasmi ya chanjo hizi. Kwa maana ktk hali ya kawaida tu huwezi kuamua kukimbilia chanjo ambazo matumizi yake yamekataliwa nchini USA na Canada, halafu leo eti zinaletwa na USA hiyo hiyo kama msaada kwa nchi yetu.
Chanjo zimezuiliwa USA na Canada? Hivi nyie watu ni nani aliyewaroga?
 
Mkuu si umeambiwa ni hiyari?
 
Haya majaribio lazima yafanikiwe maana tunao panya wa kutosha....
 
Kwanini tumeumbwa na mitazamo tofauti.
hivi hapa kusudio la alietuumba ilikuwa ni nini haswa🤔
 
Back
Top Bottom