MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Wasaidizi wa sasa wa Mheshimiwa Rais mnafeli mno, na hata wewe CDF mpya umefeli. Kwanini kuruhusu Mama kuzungumzia Siasa Jeshini? Ni hatari mno, na wenye akili kuwazidi tulidhani mngeliona hili na kumzuia asilijadili huko kwenu. Bali ajikite zaidi katika mada za kimedani (kijeshi), hasa mikakati, ulinzi na usalama ila siyo siasa, ambako MINOCYCLINE naamini huko hakukuwa mahala pake sahihi.
Rais Samia nakushauri ajiri watu wenye akili sana kuwa washauri (wasaidizi) wako, hasa huku katika Medani za Ulinzi, Mikakati na Usalama kwani uliyonao sasa hamna kitu. Wanakupotosha na watakuja kukuponza.
Ukiona nakusema jua ninakupenda.