Rais Samia kwa niaba ya wengi usiruhusu wachache waturudishe kule tulikotoka!

Rais Samia kwa niaba ya wengi usiruhusu wachache waturudishe kule tulikotoka!

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
16,950
Reaction score
13,527
Friends and Enemies,

Rais Samia,Usiwaruhusu wakufanye uwe mjinga kama jamaa yule kwenye suala hili la demokrasia,

Au pia usiwaruhusu wao wakufundishe namna gani ya kuifanya hii demokrasia ili hali wao wenyewe wanadai katiba mpya na demokrasia ili hali kwenye vyama vyao wameshindwa kuihubiri,kama wameshindwa kwenye vyama vyao wataweza vipi siku wakishika dola??mamlaka ni matamu nani asiejua??

Rais Samia,wewe una ubongo wako,fikra zako,washauri wako,vision na mission zako ya kwa namna gani utalihudumia hili taifa kwa haki bila upendeleo,so let them go to hell if what they are thinking to do is right...

Upendo na amani hauwezi kukuacha utembee pekeyako,lazima vitembee na wewe.

Ni kweli kwamba walikimbia nchi kwa mkono wa chuma ambao ulikuja kufanya exchange ya demokrasia kwa kigezo cha kufanya maendeleo,ya kwamba demokrasia inachelewesha maendeleo.

Wewe umekuja kuvifanya vyote,kurudisha demokrasia na kuendeleza maendeleo leo wanasahau wanataka kuufanya uongozi wako uhisi kuwa kumbe yule jamaa alikuwa sahihi kuwanyoosha hawa,la hasha wasikurudishe huko.

Kwenye Giza lazima kuna nuru mbele yake inakuja,tumetoka gizani na sasa tuko kwenye nuru hatuwezi kukubali wachache waturudishe tena Gizani abadani.

Kama wameshindwa demokrasia kwenye vyama vyao,kama wameshindwa kujadili kwa hoja na sasa wanataka shari na kutamani kule walipotokea,na kwamba wameyamiss sana yale maisha ni kimpango wao.

Hatuthubutu kujaribu sumu kwa kuionja,tunalinda kwanza kizuri tulichonacho kisha tutasonga mbele kwa kujiamini.
 
Hujui hata wapinzani wanalalamika nini umerukia mara, demokrasia mara kukuimbia nchi na upuuzi mwingi ulio irrelevant na malalamiko yao.
Kapotezwa Ben Saanane, Kauwawa mchana mweupe Alphonse Mawazo, Tundu Lissu kapigwa risasi lukuki,mamia ya wanachama wao wamebambikiwa kesi , wamechezewa faulo za dhahiri kwenye uchaguzi uliopita nk WAMELALAMIKA mwisho WAMENYAMAZA .
Sasa inaanzia episode TWO ya huo ubaradhuli viongozi wao wamepigwa na kudhalilishwa Mbeya na polisi Awadh, Kauwawa kiongozi wao mchana mweupe tena, wanachama wao wa Bavicha wakiongozwa na Soka wametekwa haijulikani walipo ,mikoani hali ni hiyo ukianziaa na Kombo Mbwana huko Tanga.
Unataka waendelee kunyamaza kama ng'ombe wanaingizwa machinjoni ?
We una tatizo kubwa linalokisubi kuliko unavyojua .
 
Hivi profile picture yako ni ya celebrity gani?
Inafanana na Baron Vladimir Harkonnen kwenye movie ya Dune!
 
Hujui hata wapinzani wanalalamika nini umerukia mara, demokrasia mara kukuimbia nchi na upuuzi mwingi ulio irrelevant na malalamiko yao.
Kapotezwa Ben Saanane, Kauwawa mchana mweupe Alphonse Mawazo, Tundu Lissu kapigwa risasi lukuki,mamia ya wanachama wao wamebambikiwa kesi , wamechezewa faulo za dhahiri kwenye uchaguzi uliopita nk WAMELALAMIKA mwisho WAMENYAMAZA .
Sasa inaanzia episode TWO ya huo ubaradhuli viongozi wao wamepigwa na kudhalilishwa Mbeya na polisi Awadh, Kauwawa kiongozi wao mchana mweupe tena, wanachama wao wa Bavicha wakiongozwa na Soka wametekwa haijulikani walipo ,mikoani hali ni hiyo ukianziaa na Kombo Mbwana huko Tanga.
Unataka waendelee kunyamaza kama ng'ombe wanaingizwa machinjoni ?
We una tatizo kubwa linalokisubi kuliko unavyojua .

Fuatilia vzr kitu nilichoongea.
 
Screenshot_20240918-094454.png

Yaani SSH kaona kifo cha Kibao ni kifo kama vifo vingine!
Inamaanisha michoro na mikakati ya kuteka, kutesa na kuua bado ipo mingi! Tujiandae kisaikolojia!
 
Back
Top Bottom