Rais Samia: Kwa Serikali maji si biashara, ni huduma

Rais Samia: Kwa Serikali maji si biashara, ni huduma

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Akiwa katika uwekaji Jiwe la Msingi Mradi wa Miundombinu ya Kusafisha na Kutibu Maji Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara amesema, "Kwa Serikali ndoo moja ya maji ya lita 20 inauzwa kwa Tsh. 37. Wananchi mnaonunua maji ni mashahidi dumu moja la lita 20 mnanunua Tsh. 1,000 na kwenda mbele"

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa Maji kupeleka gharama (bili) kwa Wananchi jinsi wanavyotumia, kusiwe na ubambikizaji

Aidha, amewataka Wananchi kulipa gharama za maji wanazoletelewa kwani wasipofanya hivyo mradi utashindwa kujiendesha na kupelekea wakose huduma ya Maji
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa Maji kupeleka gharama (bili) kwa Wananchi jinsi wanavyotumia, kusiwe na ubambikizaji
Kuna mtendaji wa Moruwasa Morogoro amepewa kipigo cha mbwa na askari polisi ati amebambikiziwa bill, sijui tunakosea wapi watanzania, uelewa wetu bado hafifu sana
 
Back
Top Bottom