McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Akizungumza kwenye kongamano la UVCCM la kuadhimisha miaka 62 ya Muungano Rais Samia amesema huko tunapoendea mshikamano wa kitaifa unaendelea kupungua
"Nimeacha neno mshikamano. Na hapa ndipo nataka vijana tutafakari. Neno mshikamano. Tunavyokwenda hivi, mshikamano wa Watanzania unaachia polepole.
Nadhani vijana mlioko kwenye mafunzo mmeambiwa haya, na nitakapofungua kongamano la kufunzi watalisema hili. Twendeni tutafakari sana mshikamano wa Watanzania. Na unaachia katika ngazi gani? Unaachia katika ngazi yenu vijana.
Ngazi yenu vijana mshikamano wa Watanzania unaachia polepole. Niwaombe sana vijana. Tumemsikia shehe hapa anasema hata vitabu vya dini vimesema tumewaleta ili mshikamane wala msifarakane.
Sasa vijana sasa hivi mnakuja na maneno tofauti. Kuna maneno yanaitwa 'shoti', kuna maneno sijui yanaitwa nini, mnakuja na vitaminology vidogo vidogo vya kufanya mbaguane muachane msishikamane. Hili... hili nalikemea sana vijana wangu.
Niwaombe sana rudini kwenye mshikamano. Msiharibu nchi yenu. Kamataneni, shikamaneni. Mkishikamana adui hana nafasi ya kupita. Lakini mkikubali kutenganishwa, adui mnampa njia apite. Kwa hiyo vijana wangu tushikamane ili Tanzania ibakie kuwa moja."