Rais Samia kwanini hasemi chochote popote kuhusu mambo muhimu?

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Mimi kama kuna jambo linalonishangaza kuhusu uongozi wa sasa ni ukimya wa Rais wa nchi, mambo mengi yanaendelea watu wana maswali mengi, tunapata habari tofauti, kwa nini Rais wa nchi hasimami na kuweka mambo sawa?

Kama hili la Wamasai kuondolewa kwa nini Mkuu wa nchi hatoki na kusema kuna hiki na kile, kwa nini watu wanaiongelea Serikali?

Kuna watu wanaamini kabisa Wamasai wanaondolewa kwa nguvu wakati Serikali inasema ni hiari, sasa kwa nini Rais hasimami na kuongea kumaliza mjadala?
 
Mimi kama kuna jambo linalonishangaza kuhusu uongozi wa sasa ni ukimya wa Rais wa nchi, mambo mengi yanaendelea watu wana maswali mengi, tunapata habari tofauti, kwanini Rais wa nchi hasimami na kuweka mambo sawa?

Kama hili la Wamasai kuondolewa kwanini Mkuu wa nchi hatoki na kusema kuna hiki na kile, kwanini watu wanaiongelea Serikali?

Kuna watu wanaamini kabisa Wamasai wanaondolewa kwa nguvu wakati Serikali inasema ni hiari, sasa kwanini Rais hasimami na kuongea kumaliza mjadala?
Umesharudi toka Nairobi?
 
Mimi kama kuna jambo linalonishangaza kuhusu uongozi wa sasa ni ukimya wa Rais wa nchi, mambo mengi yanaendelea watu wana maswali mengi, tunapata habari tofauti, kwa nini Rais wa nchi hasimami na kuweka mambo sawa?

Kama hili la Wamasai kuondolewa kwa nini Mkuu wa nchi hatoki na kusema kuna hiki na kile, kwa nini watu wanaiongelea Serikali?

Kuna watu wanaamini kabisa Wamasai wanaondolewa kwa nguvu wakati Serikali inasema ni hiari, sasa kwa nini Rais hasimami na kuongea kumaliza mjadala?
Rais SSH Kaamua maneno yawe machache vitendo ndio viongee. La Loliondo limekuwepo tangu awamu ya pili ya Mzee Mwinyi kaamua kulimaliza kabisa.

La wamachinga lilikuwa likiondoka na kurudi akaamua kulimaliza mazima. Hana mikwara ya kutokwa mapovu mpaka mishipa ya shingo ijitokeze usoni.
 
Hiyo siyo leadership, kama wananchi unaowaongoza hawaelewi nini kinaendelea Kiongozi anapaswa kuongea na kuongea maana yake siyo kutokwa povu, bali unaweza kuongea kwa kawaida tu!
 
Wangekuwa hawaelewi nini kinaendelea wasingekuwa kimya wakiridhika na kinachoendelea. Huu ndio uongozi matumizi ya akili na nguvu vinakwenda sawa.
 
Ndio maana Ikulu kuna msemaji mkuu na mtu wa habari hao wapo kwa ajili ya kumuongelea Rais, je siku tukiwa na Rais bubu utamlazimisha aongee.

Rais anaongea pale inapobidi
 
Ndiyo, kuna namna ambayo Bubu anaweza kufikisha ujumbe kwa walengwa, btw kwa hiyo walioweka hotuba kwa Maraisi wote Duniani walikuwa ni wajinga kama raisi hana haja ya kutolea ufafanuzi jambo lolote kwa kuwa ana wasaidizi?
 
Ndio maana mwisho nikasema Rais anaongea pale inapobidi km vile kuhutubia Taifa ila sio mropokaji wa kila jambo linalotokea yeye akurupuke aongee hapo ataharibu kwa hiyo muache kwanza atafakari haya yanayojiri atakuja kuyaongea kwa summary
 
Hiyo siyo leadership, kama wananchi unaowaongoza hawaelewi nini kinaendelea Kiongozi anapaswa kuongea na kuongea maana yake siyo kutokwa povu, bali unaweza kuongea kwa kawaida tu!
Raisi wa nchi haropokiropoki. Uraisi ni taasisi hata akiongea IGP tu kuongea raisi.
 
Rais
Hajalizungumzia kwa sababu halijafikia kuwa big issue mpaka Rais alizungumzie mkuu.

Kwa sasa bado liko ngazi ya kuzungumziwa na MKUU WA WILAYA, MKUU WA MKOA,, IGP Na wengine viongozi.

Na hao wote wameshalizungumzia akiwepo na Waziri Mkuu.

Kwa Hiyo mkuu ukiona Rais yuko kimya Juwa si big issue inayohitaji mpaka Rais aongee.

MWISHO.

Pitia mitandao na hutuba mbalimbali mbona limeshazungumzwa sana.

Pia, labda kama pia halijazumzwa Public labda si sehemu ya wote kulijuwa ila Wahusika wa LOLIONDO naamini wana Taarifa za kutosha kuhusu hili.

HAYO NI MAONI YANGU TU.
 
Mayeroo watahama tu kwa hiyari au shurti. Wao sio jamii ya kwanza kuhamishwa nchini, kila siku watu wanahama kwa maslahi mapana ya taifa, kama wao wanajiona special sana basi watakipata wanachokitafuta.
 
Mimi kama kuna jambo linalonishangaza kuhusu uongozi wa sasa ni ukimya wa Rais wa nchi, mambo mengi yanaendelea watu wana maswali mengi, tunapata habari tofauti, kwa nini Rais wa nchi hasimami na kuweka mambo sawa?

Kama hili la Wamasai kuondolewa kwa nini Mkuu wa nchi hatoki na kusema kuna hiki na kile, kwa nini watu wanaiongelea Serikali?

Kuna watu wanaamini kabisa Wamasai wanaondolewa kwa nguvu wakati Serikali inasema ni hiari, sasa kwa nini Rais hasimami na kuongea kumaliza mjadala?
Siyo mambo yote aseme rais kuna wizara.
 
Back
Top Bottom