Rais Samia kwanini unafanya hivi? Ni wapi tumekukosea?

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Mama Samia kwa nini mnafanya hivi, mbona hii sio fair? Ni wapi tumekukosea?

Kabla nilitegemea ulipoingia ungepunguza ukali wa maisha Ila ukali ndio unazidi.

Mama Samia mbona hakuna aliyekataa kulipa Kodi?

Ndani ya miezi minne kufanya haya mabadiliko makubwa hivi huoni ni kama unatutesa sana?

Hebu tuambie Hawa watangulizi wako mbona walijenga nchi bila hizi tozo?

Mama Samia mboma JK alijenga shule za kata nchi nzima bila kuongeza tozo?

JK alijenga barabara kuunganisha mikoa yote bila tozo hizi

Mbona Magufuli kajenga hizo hospital bila tozo?

Mbona Magufuli kajenga hayo madaraja na flyover bila hizi tozo?

Leo hii kila kitu kimepanda bei hadi nyama buchani imepanda

Mama ni kwamba hujui Watanzania walio wengi wana maisha duni sana?

Watanzania wengi wanategemea kilimo huko napo mbolea imeongezeka Bei Mara mbili.

Swali langu mama mbona ni muda mfupi sana haya mabadiliko ya maisha?
 
Hataki kuongeza mishahara na kupandisha madaraja wafanyakazi, hapo hapo anataka akamue tozo kila eneo, hii Tanganyika inahitaji kuongozwa na watanganyika wenyewe. Tusipotezeane uelekeo, tunahitaji katiba mpya sasa.
 
Uchaguzi ulikua mzuri sana! Tumepita na kushinda Kwa kishindo kikubwa! Tulipe Kodi Kwa maendeleo yetu
 
Reactions: Qwy
Utasikia 2025 aki tubembembeleza nchi nzima
 
Hataki kuongeza mishahara na kupandisha madaraja wafanyakazi, hapo hapo anataka akamue tozo kila eneo, hii Tanganyika inahitaji kuongozwa na watanganyika wenyewe. Tusipotezeane uelekeo, tunahitaji katiba mpya sasa.
Anaetaka kuongezewa mshahara ahamie Burundi.
CCM mbele kwa Mbele..!
 
Anaetaka kuongezewa mshahara ahamie Burundi.
CCM mbele kwa Mbele..!
Tumeshachaguliwa na nchi ya kwenda, waliokuwa wanajitapa kwamba watadandia ndege ya biden kwenda marekani watajikuta wametupwa hapo bujumbura...
 
Mkuu huu ushaur ungeuandik kwa wanaomshaur dodoma pale ... Naona first class z Udsm zinaporomosh maumiv ya first grade kw wanyonge [emoji28]
Hicho chuo kimeifikisha hapa Tanzania.
 
Mkuu,mmeshaambiwa maisha yakiwashinda mhamie Burundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…