Rais Samia kwanini unafanya hivi? Ni wapi tumekukosea?

Rais Samia kwanini unafanya hivi? Ni wapi tumekukosea?

Hizi tozo ni uharamia!! Watueleze vizuri. Kodi tumelipa! Matumizi mengi yamepanda kuanzia July!
Tozo zinatokana na fedha binafsi za watu ni kosa kubwa ni unyanganyi!!

Tunataka katiba mpya!!!!

Tunataka majimbo ya wabunge yapungue
Tunataka wabunge covid 19 waondolewe,
Tunataka wakuu wa wilaya waondolewe kupunguza gharama,
Kwenye mikoa na wilaya kuna wakuu wa idara, wakurugenzi, maDC, wakuu wa mikoa, RAS,
DAS, Makatibu wakuu, sehemu nyingine na mayors,!!!
Wote hawa wanapewa mashangingi, mafuta, matengenezo ya magari, allowances chungu bovu!!!
Hivi wote hawa wapo huko chini lakini bado utaona...,.
Bado utaona mawaziri wanazunguka,
Mawaziri manaibu wanazunguka,
Waziri mkuu anazumguka,
Katibu mwenezi wa ccm anazunguka!
Katibu mkuu wa ccm anazunguka,
Deputy President anazunguka!
Rais naye anazunguka!!
Mikutano kedekede kila siku iliyo na misururu ya magari yasiyopungua hamsini!!!
Kama hawa wote walioko chini hawatoshi faida yao ni nini???

Tunahitaji katiba mpya ili tusahahashe makosa haya!! Unyonyaji huu!!

Hatuwezi kutwisha wananchi gharama zisizo muhimu!!!

Wote wazungukaji wanatumia petrol!
Magari yanahitaji matengenezo,
Watu wote wanaposafiri wanahitaji posho za kujikimu nazo ni kubwa sana,

Viongozi wakiwa juu wanajikusanyia mali nyingi na bado wakistaafu wanalipwa mishahara na kulindwa na sasa wameongeza kujengewa nyumba za fahari kando ya bahari!!
Mitaji ya watawala wa ccm ni unyonge wa watanzania!
Ujinga wa watanzania!
Uwoga wa watanzania,
Elimu duni ya kitanzania,

Watanzania amkeni sote tufaidike!!
Ccm imekuwa mali ya familia!!
Amina!!
 
Mama Samia kwa nini mnafanya hivi, mbona hii sio fair? Ni wapi tumekukosea?

Kabla nilitegemea ulipoingia ungepunguza ukali wa maisha Ila ukali ndio unazidi.

Mama Samia mbona hakuna aliyekataa kulipa Kodi?

Ndani ya miezi minne kufanya haya mabadiliko makubwa hivi huoni ni kama unatutesa sana?

Hebu tuambie Hawa watangulizi wako mbona walijenga nchi bila hizi tozo?

Mama Samia mboma JK alijenga shule za kata nchi nzima bila kuongeza tozo?

JK alijenga barabara kuunganisha mikoa yote bila tozo hizi

Mbona Magufuli kajenga hizo hospital bila tozo?

Mbona Magufuli kajenga hayo madaraja na flyover bila hizi tozo?

Leo hii kila kitu kimepanda bei hadi nyama buchani imepanda

Mama ni kwamba hujui Watanzania walio wengi wana maisha duni sana?

Watanzania wengi wanategemea kilimo huko napo mbolea imeongezeka Bei Mara mbili.

Swali langu mama mbona ni muda mfupi sana haya mabadiliko ya maisha?
Tozo ziendelee maana tumekuwa mazombi
 
Back
Top Bottom