Rais Samia: Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani

Rais Samia: Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kifo cha Mafuru kimeibua mambo mengi kwa kweli kwenye eneo la uchumi.

Huyu Mzee alifanya yake kwenye kipindi cha changamoto wa upatikanaji wa dola. Pumzika kwa amani

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza namna, Lawrence Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani hatua ambayo imechochea nchi kujiimarisha.

Amesema wakati wa changamoto hiyo, Mafuru alikuwa miongoni wa wajumbe wa kamati wa kushughulikia changamoto ya Dola na aliifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.

“Tulipopata changamoto ya Dola niliunda kamati ya kushughulikia suala hilo, kamati iliongozwa na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu akisaidiwa na wengine akiwemo Mafuru.

“Nakumbuka siku ya kutoa wasilisho lao, Mafuru aliniambia tukiufuata huo mkakati tutaondokana kabisa na hiyo changamoto ya dola na hicho ndicho kilichotokea,” amesema Rais Samia.

Soma Pia:
Kando na hilo, pia Rais Samia amegusia namna Mafuru alivyokuwa akitoa ushauri katika mambo mbalimbali ambayo yaliisaidia nchi kujikwamua.

Rais Samia amebainisha hayo leo Alhamisi Novemba 14, 2024 alipoongoza viongozi mbalimbali kuaga mwili wa Lawrence Mafuru, aliyefariki Novemba 9, 2024 nchini India, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 
Back
Top Bottom