Rais Samia: Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani

Rais Samia: Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani

Kifo cha Mafuru kimeibua mambo mengi kwa kweli kwenye eneo la uchumi.

Huyu Mzee alifanya yake kwenye kipindi cha changamoto wa upatikanaji wa dola. Pumzika kwa amani

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza namna, Lawrence Mafuru, alivyoinusuru nchi na changamoto ya uhaba wa Dola ya Marekani hatua ambayo imechochea nchi kujiimarisha.

Amesema wakati wa changamoto hiyo, Mafuru alikuwa miongoni wa wajumbe wa kamati wa kushughulikia changamoto ya Dola na aliifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.

“Tulipopata changamoto ya Dola niliunda kamati ya kushughulikia suala hilo, kamati iliongozwa na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu akisaidiwa na wengine akiwemo Mafuru.

“Nakumbuka siku ya kutoa wasilisho lao, Mafuru aliniambia tukiufuata huo mkakati tutaondokana kabisa na hiyo changamoto ya dola na hicho ndicho kilichotokea,” amesema Rais Samia.

Soma Pia:
Kando na hilo, pia Rais Samia amegusia namna Mafuru alivyokuwa akitoa ushauri katika mambo mbalimbali ambayo yaliisaidia nchi kujikwamua.

Rais Samia amebainisha hayo leo Alhamisi Novemba 14, 2024 alipoongoza viongozi mbalimbali kuaga mwili wa Lawrence Mafuru, aliyefariki Novemba 9, 2024 nchini India, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Obsession ya Waziri wa Fedha itaisha lini … Ameshindwa kabisa hata KUMZIKA?? ; inajulikana wazi kuwa alikuwa anamuona tishio kwa kazi yake … hatujamuona kabisa … ka post picha moja tu kinafiki

TUNAJUA …
 
Mbona Kila siku walikuwa wanasema hakuna changamoto yoyote ya dollar tuna reserve ya kuhudumia east Africa kwa kipindi cha miezi sita..........!
Technically ilikua ni kupunguza taharuki kwa jamii! Na imefaulu kwa kiasi chake!!
 
Technically ilikua ni kupunguza taharuki kwa jamii! Na imefaulu kwa kiasi chake!!
Huu ndio ungedere wenyewe sasa aka apedonia ,huwezi solve tatizo kwa kuchimbia kichwa kwenye mchanga ukijidanganya kwa kusema kwamba tatizo halipo wakati tatizo lipo .
Hizi ni akili za bata .
Taaruki taaruki gani ? ,Hii nchi serikali inafanya wananchi kama misukule ,kufanya mambo kama waganga wa kienyeji .
Kila mtu kitaa anajua siku zote dollar haipatikani ni mwaka sasa na hata sasa hali bado haijawa nzuri ,sasa wanaficha nini

Rubbish
 
Hii kauli maana yake ni kuwa Waziri wa fedha hana msaada na siku zake zinahesabika 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom