kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Rais samia hua anatoa kauli na maelekezo yenye utata. Lakini wenye kuelewa wanajua ni mwelekeo wake wa kupendelea sekta binafsi iliyojaa 'wahuni'
Inafaa atambue sekta binafsi kuleta ufanisi inatakiwa kua shindani sio kubebwa kwa kusudi kuingia ubia na majeshi au mashirika au mamlaka za umma ambapo makomanda na vigogo wanagombea ulaji na wala weledi hawana.
Anapaswa kutambua majeshi wakati wa amani lazima kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Mtangulizi wake alitaka jeshi la magereza kutumia wafungwa kuzalisha mali na kwanza kabisa kujitegemea kwa chakula.
Kama Rais anazo taarifa za mifarakano kwenye miradi ya magereza kwa nini asitake kujua wakorofi au wakwamishaji akawatumbua. Nidhamu ya kijeshi na weledi ndio jambo muhimu kupata ufanisi.
Kutaka makomanda wa magereza wanaovutana kugombea ulaji kwenye miradi waingie ubia na sekta binafsi hapo ni kuanzisha ushirikiano wa makamanda wasio waadilifu wa magereza na 'wahuni' ambapo fedha ya umma italiwa na kutajirisha fisadi tu.
Rais samia ajue hawezi kufanikiwa kwa kutafuta sifa kwa mabwanyenye wabinafsi wenye nia siku zote kupiga hela ya umma kwa ushirika na serikali. Ushirika usiyokua na tija kwa umma wa wananchi.